NYOTA NDOGO:

Baby wangu ana wivu hatari

Mtanzania - - Swaggaz - NAIROBI, KENYA

STAA wa muziki nchini Kenya, Nyota Ndogo amedai mpenzi wake Henning Nielsen, raia wa nchini Denmark, ana wivu ambao hajawahi kuuona. Msanii huyo wiki chache zilizopita alikuwa nchini Denmark kwa mume wake mtarajiwa na mara baada ya kurudi Kenya alitangaza ratiba yake ya ziara ya muziki, hivyo baada ya mpenzi wake kusikia kuwa Nyota Ndogo anataka kufanya ziara ameamua kupanda ndege na kutua Kenya. Msanii huyo amesema mpenzi wake huyo amekuja ghafla baada ya kumpa taarifa ya ziara yake nchini Kenya, hivyo ni wivu ambao umemfanya aje kuzunguka na mrembo huyo.

“Nimetoka wiki chache zilizopita nchini Denmark, lakini baada ya kumpa taarifa kuwa nataka kufanya ziara ya muziki hivi karibuni naona amefunga safari ili tuje kuwa wote kwenye mizunguko yangu, hii ni sehemu ya wivu ambayo sijawahi kuuona, lakini hii ni sehemu ya kupendwa,” aliandika Nyota Ndogo.

Hata hivyo baadhi ya mashabiki wa msanii huyo wametoa maoni yao wakimponda jamaa huyo, raia huyo wa Denmark wakidai kuwa hana lolote na kwamba akishamaliza haja zake atamtelekeza mrembo huyo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.