Trump abeza uteuzi wa kumchunguza

Mtanzania - - Kimataifa -

RAIS Donald Trump wa Marekani amebeza uteuzi wa mwanasheria maalumu kuchunguza kampeni yake inayohusishwa na udukuzi wa Russia.

Uchunguzi huo unafungamana na uchaguzi wa rais mwaka jana, Trump akisema hatua hiyo ni “tukio la namna ya kipekee katika kumtafuta mchawi lililoelekezwa kwa mwanasiasa katika historia ya Marekani.”

Trump alikuwa ametatizika Jumanne baada ya kuteuliwa Robert Mueller, aliyekuwa mkurugenzi wa FBI, kuongoza uchunguzi ili ifahamike iwapo kati ya wasaidizi wa Trump yupo aliyevunja sheria kwa kushirikiana na maofisa wa Russia katika juhudi za kumsaidia Trump kupata nafasi ya ushindi katika uchaguzi wa urais mwaka jana.

Katika maoni yake mapema asubuhi katika akaunti ya Twitter, Trump amelalamika kuwa, mchunguzi maalumu hajawahi kutajwa kuchunguza “vitendo vyote vya uvunjaji sheria vilivyotokea” katika kampeni ya uchaguzi wa mpinzani wake wa Chama cha Demokratik, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton na uongozi wa aliyemtangulia wa Rais Mstaafu, Barack Obama.

Rais amesema pamoja na vitendo vyote vilivyokuwa kinyume cha sheria vilivyotokea katika kampeni ya Clinton na Uongozi wa Obama, hakukuwa na mwanasheria maalumu aliyeteuliwa kuchunguza!

SHERIA: Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali ya Sweden, Marianne Ny, akitangaza uamuzi wa kufutwa mashtaka ya ubakaji jana, ambayo yalikuwa yakimkabili mwanzilishi wa mtandao wa WikiLeaks, Julian Assange.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.