Rais mpya Ufaransa aanza ziara Afrika

Mtanzania - - Kimataifa -

RAIS mpya wa Ufaransa, Emmanuel Macron, ameanza rasmi ziara yake ya kwanza barani Afrika juzi, tangu kuchaguliwa kwake. Rais huyo anatarajiwa kuzuru Mali, ambako atakutana na kikosi cha askari wa Ufaransa wa operesheni Barkhane.

Kwa sababu za kiusalama, taarifa za ziara ya rais huyo nchini Mali hazijulikani. Lakini anatarajiwa kutembelea mji wa Gao, uliopo kaskazini mwa Mali. Katika eneo hilo ndipo kunapatikana idadi kubwa ya askari wa Ufaransa wanaoendesha Operesheni ya Barkhane.

Askari wa Operesheni Barkhane wanakadiriwa kuwa 4,000 katika nchi tano za ukanda wa Sahel. Kikosi hiki kiliundwa mwaka 2013, baada ya askari wa Ufaransa kuingilia kijeshi kuzuia wanamgambo wa Kiislamu waliokuwa wakisonga mbele katika maeneo mbalimbali ya kivita kusini mwa Mali.

Hata hivyo, wanamgambo hao bado wanaendelea kuhukumu raia nchini humo, na askari wa Ufaransa wanaendelea na mapambano dhidi ya makundi hayo.

Lengo la rais mpya wa Ufaransa ni kukutana na askari wa Ufaransa kama amiri jeshi mkuu. Aidha, Rais Macron atakutana na mwenzake wa Mali, Ibrahim Boubacar Keïta.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.