Singida United wafichua siri ya usajili

Mtanzania - - Michezo - Na ZAINAB IDDY - DAR ES SALAM

UONGOZI wa timu ya Singida United umesema mpango wao ni kuwa na wachezaji wanaojua majukumu yao na wengi ni wale wanaochezea timu zao za taifa kwenye nchi wanazotoka.

Singida United, iliyopanda Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, imefanya usajili wa wachezaji wanne wa kigeni, ambao wote wanazitumikia timu zao za taifa.

Kikosi hicho kinachotarajiwa kuwa chini ya kocha Hans van der Pluijm, aliyewahi kuinoa Yanga, kimeshaingia mikataba ya miaka miwili na wachezaji hao kwenye timu zao za taifa; Elisha Muroiwa, Wisdom Mtasa na Tafadwaza Kutinyu, ambao wote ni Wazimbabwe pamoja na Shafik Batambuze, raia wa Uganda.

Mratibu Mkuu wa Singida, Festo Sanga, ameliambia MTANZANIA Jumamosi kuwa, siri kubwa ya kusajili wachezaji wanaotoka timu za taifa ni uzoefu na changamoto nyingi za uwanjani, tofauti na wale ambao hawajawahi kucheza timu za taifa.

“Hadi sasa tumesajili wachezaji wanne wa kigeni na kubakiwa na watatu ambao nao ni wale wanaopata nafasi kwenye timu zao za taifa, hata kama tutawasajili wanaocheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara, na hili tunalifanya pia hata kwa wachezaji wazawa, sharti letu lazima wawe wanaitwa kuitumikia Taifa Stars kimataifa,” alisema.

DANADANA: Bingwa wa dunia wa mpira wa miguu (Freestyle Football Tanzania) raia wa Japan, Kotaro Tokuda, akionyesha mbwembwe jijini Dar es Salaam jana katika ziara yake iliyodhaminiwa na Redbull Tanzania.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.