Mayanga aita 24 Stars ya kwenda Misri

Mtanzania - - Michezo - Na MWANDISHI WETU

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ Salum Mayanga ametangaza majina ya wachezaji 24 watakaounda kikosi hicho kinachodhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti.

Kikosi hicho kitaingia kambini Jumanne kwenye Hoteli ya Urban Rose, Dar es Salaam hadi Mei 29 na itasafiri kwenda Misri kwa kambi ya wiki moja kabla ya kurejea kucheza mchezo wa kufuzu Mataifa ya Afrika na Lesotho, Juni 10 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mayanga alisema kikosi hicho kinaundwa na makipa Aishi Manula (Azam FC), Benno Kakolanya (Yanga SC) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar). Walinzi wa pembeni upande wa kulia, Shomari Kapombe (Azam FC) na Hassan Kessy (Yanga SC) wakati upande wa kushoto wapo Mohammed Hussein (Simba) na Haji Mwinyi (Yanga SC).

Walinzi wa kati Erasto Nyoni (Azam FC), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Aggrey Morris (Azam FC) huku viungo wa kuzuia ni Himid Mao (Azam FC) na Jonas Mkude (Simba SC).

Viungo wa kushambulia Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla (Simba SC) na Muzamiru Yassin (Simba) wakati viungo wa kulia Simon Msuva (Yanga SC) na Shizza Kichuya (Simba SC).

Viungo wa kushoto ni Farid Mussa (Teneriffe, Hispania) wakati washambuliaji ni Mbwana Samatta (KRC Genk- Ubelgiji), Thomas Ulimwengu (AFC Eskilstuna – Sweden), Ibrahim Ajib (Simba SC), Mbaraka Yusufu (Kagera Sugar) na Abdurahman Mussa (Ruvu Shooting). Kocha msaidizi ni Novatus Fulgence wakati kocha wa makipa, Patrick Mwangata, Meneja Danny Msangi, Mtunza vifaa, Ally Ruvu na Daktari wa timu Richard Yomba huku Daktari wa viungo ni Gilbert Kigadya.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.