Wenger: Nne bora si muhimu kabisa kwa Arsenal

Mtanzania - - Michezo -

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema timu ya Arsenal kumaliza nne bora si jambo la muhimu sana, na anashangaa kwa nini mashabiki wanaona ni jambo la maana sana.

Arsenal waliongeza tumaini lao la kutinga nne bora baada ya Jumanne iliyopita kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sunderland, mabao yote yakiwekwa kimiani na mshambuliaji wao, Alexis Sanchez.

Pamoja na ushindi huo, bado Arsenal ipo kwenye vita dhidi ya Manchester City na Liverpool ya kubakia kwenye nafasi ya nne wakati wakicheza michezo yao ya mwisho ya kumaliza rasmi msimu huu.

Hata hivyo, kuyumba kwa timu ya Arsenal msimu huu kunaonekana kuwakera zaidi mashabiki wa timu hiyo, wakitaka Wenger aondoke. Mabango yamekuwa yakirindima takribani kila mchezo kumtaka Mfaransa huyo kuondoka katika klabu hiyo, kwani mashabiki wengi hawakubaliani na kiwango cha timu hiyo.

Kibaya zaidi ni kauli aliyoitoa Mfaransa huyo kuhusu jitihada zao kumaliza nne bora msimu huu, Wenger aliwaambia mashabiki wa Arsenal kuingia nne bora “si jambo muhimu”.

Wenger anashangaa kwanini watu wanaona nne bora ni jambo kubwa? “Huwezi kufahamu tutaishia wapi lakini swali hili nimekuwa nikilijibu sana kwamba kutinga nne bora si jambo la maana sana,” alisema Wenger.

Wenger alisema suala la mashabiki kujadili wao kutoingia kwenye nafasi hiyo, linamshangaza kwa sababu haoni kama lina uzito, aliongeza watapambana kupata nafasi nne za juu, lakini hata wakishindwa haliwezi kuwanyong’onyeza.

Arsenal wana pointi 72, huku Liverpool wanaoshika nafasi ya 4 wakiwa na alama 73 na hii inamaanisha kwamba Liverpool wakishinda katika mchezo wao wa mwisho itawafanya Arsenal kumaliza nafasi ya 5 msimu huu.

Wenger

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.