FUNGA KAZI LIGI KUU BARA

Timu mbili kuifuata JKT Ruvu FDL

Mtanzania - - Michezo -

TIMU ya Yanga leo inafunga pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara, ikiwa imejihakikishia ubingwa wa ligi hiyo kwa kumenyana na Mbao FC katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza leo. Yanga inaingia uwanjani ikiwa tayari imeshatangaza kutetea taji hilo, baada ya kushinda bao 1-0 dhidi ya Toto Africans Jumanne iliyopita katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga imefikisha pointi 68, huku watani wao wa jadi, timu ya Simba wakishika nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 65.

Simba itahitajika kushinda mabao zaidi ya 10-0 dhidi ya Mwadui katika mchezo wao wa mwisho utakaochezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ili waizuie Yanga kutwaa ubingwa huo.

Lakini matokeo hayo yatakuwa na faida kwa Simba ikiwa Yanga watafungwa na Mbao FC kwenye mchezo wao leo, jambo ambalo linaweza kuwa gumu kwa Simba kuwafunga mabao mengi wapinzani wao.

Iwapo Yanga itaifunga Mbao au Simba kushindwa kufikisha idadi hiyo ya mabao dhidi ya Mwadui, watakuwa wamewapa nafasi

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.