Chakula ndiyo kila kitu, wekeza katika kilimo

Mtanzania - - Habari - Kinachoweza kuwaongezea kipato.

CHAKULA ni kile kinacholiwa na watu kwa kudumisha maisha yao. Mwili unahitaji virutubishi, nishati na maji ambavyo vyote hupatikana katika chakula kinachotoka kwenye mimea na wanyama Virutubishi vya mwili ni pamoja na protini, mafuta, wanga, vitamini na madini. Protini, mafuta na wanga huleta nishati ya mwili. Vilevile hukuza mwili yaani katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula (tumboni) zinapasuliwa kwa sehemu asilia zao na kuingizwa katika muundo wa seli za mwili.

Kutokana na hali hiyo umuhimu wa kilimo unaonekana dhahiri katika maisha ya binadamu.

Nchi za Afrika ikiwamo Tanzania zimejaliwa kuwa na ardhi nzuri yenye rutuba lakini bado wakulima wengine hawaoni matokeo mazuri ya shughuli hiyo.

JIONGEZE lilifanya mahojiano maalumu na Ofisa Masoko wa Kampuni ya Usambazaji wa Vifaa vya Kilimo ya Lonagro Tanzania Ltd, Godfrey Byabato.

Ofisa huyo anataja sababu ya kufeli wakulima wengi katika kilimo.

Anasema wakulima wengi katika nchi za Afrika bado ni wadogo, wanalima kwa ajili ya chakula na kiwango wanachozalisha ni kidogo kinachotosha kwa ajili ya chakula cha familia na si kilimo biashara

“Ajira kubwa kwa Afrika sasa hivi ipo katika kilimo, ndiyo inayoajiri watu wengi zaidi tofauti na nchi za Ulaya ambao wana viwanda na vitu vingi ambavyo wanaweza kujihusisha navyo.

“Endapo mkulima atajiingiza kwenye kilimo biashara anatakiwa kuwa na nyenzo bora ambavyo ni vifaa vya kisasa.

“Leo ukisema watu wachague kipi muhimu kati ya madini na chakula kila mmoja atachagua chakula, hapo ndipo unapoona thamani ya chakula hivyo wakulima wanatakiwa kuweka ukubwa wa thamani wanayoweka kwenye madini iende kwenye kilimo kwa kuwa na nyenzo muhimu,” anasema.

Anasema si kwamba wakulima wanapenda kufanya kilimo ambacho si cha kisasa kwa kutumia matrekta na mashine zake ila ni kwa sababu uwezo wa kununua kwa fedha taslimu ni mdogo.

Kutokana na kuona changamoto hiyo, kampuni hiyo imekuwa na utaratibu wa kuwasaidia wakulima kupata matrekta na kulima kisasa.

“Tuna programu inayoitwa ‘Rent to Own’ ambayo tunawasaidia wakulima ambao hawakopesheki na benki kutokana na kutokikidhi vigezo vinavyowekwa.

“Mfumo wake ni wa mkopo wa muda mfupi am- bao unaweza kumsidia mkulima kukopa vifaa ya kilimo kwa mahitaji hivyo pasipo kumbana anatakiwa kuwa malipo ya awali ya asilimia 35 ya ile bei ya kifaa, asilimia ambayo kwa wakulima wengi wanaimudu.”

Anasema kitu kingine anachotakiwa kuwa nacho ni kitambulisho cha kupigia kura, kitambulisho cha uraia, leseni pia awe na barua ya utambulisho wa makazi yake, anaishi wapi na anapokwenda kufanya kilimo.

Anasema anatakiwa kutambuliwa na mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa anaoishi, majirani wa mtaa ule wanamtambua na akishajaziwa hivyo fomu ndio anakidhi vigezo ya kupata trekta.

“Ni mkopo wa muda mfupi ambao ni miezi tisa tu na tunakopesha trekta pekee yake, mashine nyingine ananunua na kwa kuwa ni bei ndogo kuliko trekta.

“Hatukopeshi vifaa vingine kwa kuwa havijidhamini ikilinganishwa na trekta inajidhamini yenyewe na kuwa huwa wanabaki na kadi ya trekta hadi mkulima anapomaliza deni ingawa trekta anakuwa analitumia.

Anasema kwa kuwa mkulima anakuwa ametoa asilimia 35 anajitahidi kumaliza ili aweze kumiliki trekta na kadi.

Anasema ili maisha yawe safi na uchumi wa mkulima ukue ni lazima afanye kilimo biashara na si kupata chakula peke yake.

Anasema katika kuhakikisha wanawasidia wakulima pia wana ushirikiano na taasisi nyingine wanaosaidia wakulima wadogo wadogo katika mikopo ili wakue.

Anasema wameingia makubalinao na benki ya NMB, EFTA, mfuko wa pembejeo wa taifa na hivi karibuni walifanya mazungumzo na taasisi ya Pass.

Anasema ni vyema vijana wajiajiri katika kilimo biashara kwa kuwa Serikali haiwezi kuajiri watu wote.

“Tuna watu wanaomaliza vyuoni na hawana ajira, kilimo ndiyo fursa pekee iliyobaki kwa sababu Waafrika tuna ardhi nzuri, mtu akijiingiza kufanya kilimo biashara inalipa zaidi.

Changamoto wanazokumbana nazo katika masoko anasema zipo nyingi moja za kimazingira na nyingine ni za kiuchumi na pia zipo zinazosababishwa na binadamu si za mazingira na kiuchumi.

Anasema uelewa wa wakulima bado ni mdogo na tumekuwa tukitumia nguvu kubwa kuwaeliemisha wakulima kuwa wanaweza kumiliki trekta.

Anasema katika matumizi wengi hawajui kuvitumia kwa usahihi, wanatumia vibaya lakini baada ya muda kinapoharibika anakuja kulalamika kuwa umemuuzia kitu kisichofaa.

Pia anasema kuna changamoto za uchumi ambao unapanda na kushuka.

Ni mkopo wa muda mfupi ambao ni miezi tisa tu na tunakopesha trekta pekee yake, mashine nyingine ananunua na kwa kuwa ni bei ndogo kuliko trekta.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.