Unawakumbuka ‘The bebst dancers’ 1992

Mtanzania - - Swaggaz - Na Jimmy Chika +255 0783 017 111 Jimmy Chika ni Mhariri wa gazeti la Dimba, mbobezi wa uchambuzi wa muziki wa vijana wa zamani. 0783 017 111

UKIRUDISHA fikra zako nyuma hadi mwaka 1982, na kama ulikuwa mkazi wa Jiji la Dar es salaam, au ulikuwa mdau wa muziki wa diusko basi hutoacha kuyakumbuka majina ya wacheza disko maarufu enzi hizo.

Kadhalika hutoacha kuzikumbuka kumbi zilizotumika sana mniaka hiyo kwa ajili ya maonyesho na mashindano ya disko yaliyopata kupata umaarufu mkubwa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Leo tunayakumbuka mashindano makubwa ya disko yaliyokuwa na hadhi ya kitaifa na hata babbadhi yaliyokwenda mbali zaidi na kuwakilisha washiundani toka nchi za Afrika Mashariki enzi hizo Uganda, Kenya na Tanzania.

Licha ya nchi ya Kenya kuwa na mchweza disko hata kipindi hicho aliyejulikana kwa jina la Kanda Kid lakini hapa Tanzania majina yalikuwa mengi na hata uchezaji wao ulikuwa wenye sifa kubwa ulioitangaza vizuri nchi yetu.

Mathalan alikuwepo kijana Musa Simba au akifahamika zaidi kama Black Moses, ambaye enzi hizo alistaajabisha mashabiki kutokana na uwezo wake wa kunyonga viungo vyake na akionekana kucheza kama kwambba hakuwa na mfupa.

Si yeye tu bali walikuwepo wengine kama Athumani Mitikasi, Supert Jobiso, Kiss Ngedele, Bosco Coll J, Ashura Mponda au Qeen Clouds, Elvis Danger, Banza Stone, Elvis Danger, Ommy Kiss,Max Prinst, Chino Loketo, Peter Disco Wizard, Mc Chunusi na wengine wengi.

Hawa walitamba sana katika miondoko ya disko hasa wakati uler walicheza nyimbo za wanamuziki maarufu duniani kama vile Michael Jackson, Tinner Tunner, Colnel Abraham, Lady Madona na wengine wengi kwa hakika walizitendea haki nyimbo za wanamuziki hao na wengine ambao kwa haraka sikuwakumbuka.

Ukiacha aina hiyo ya wanenguaji lakini lipo kundi ambalo kwao walijijengea umaarufu sana kwa uchezaji wa mitindo ya Kiafrika, hususan kutoka nchi ya DRC ambapo enzi hiyto ilikuwa ikjulikana kama Zaire.

Mitondo ya Kwasakwasa, Ndombolo Yasolo, Soto, Mayenu na mingine ambayo ilitokea kaauwa maarufu sana katika ukanda huu wa Afrika.

Wanamuziki kama Kanda Bongo Man, Mayaula Mayaono, Kabasele Pepe Kale, Aurus Mabere, Joen Bokilo, Bozi Boziana na wengine kadhaa waliwafanikiwa kujikusanyia idadi kubwa ya mashabiki karibu kila kona ya Afrika.

Katika Jiji la Dar es salaam kulikuwa na wachezaji maarufu wa mitindo hiyo ambao wengi kati yao walikuwa wanamuziki lakini waliojikita zaidi katika unenguaji.

Yapo majina kama Masengo Nduka au Malick Star, Nyota Kinguti, Bobo Sukari, Fredito Butamu na wengine wengi nao walikuwa wakiumana vikali katika mashindano mbalimbali ya disko.

Kwa hakika baada ya kuondoka makaundi haya, sanaa ile ya ugenguaji japokuwa inaendelea lakini siyo katika viwango, hivi sasa ubunifuaa umekuwa mdogo kuliko biashara.

Mbaya zaidi wanenguaji wanaoitumia vibaya tasnia hiyo nao wamengezeka maana sasa wapo wanaocheza nusu utupu majukwaani wakionekana kama wenye nia yua kuonyesha burudani hiyo kumbe wanafanikisha nia zao nyingine.

Ndiyo mana hadi leo bado tunawakumbuka wasanii wale ambao wengi kakti yao wameshaaga dunia na waliobaki wamekuwa watu wazima wanaojihusisha na shughuli nyingine za kijamii.

Leo tunayakumbuka mashindano makubwa ya disko yaliyokuwa na hadhi ya kitaifa na hata babbadhi yaliyokwenda mbali zaidi na kuwakilisha washiundani toka nchi za Afrika Mashariki enzi hizo Uganda, Kenya na Tanzania.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.