Izzo Bizness ampa zawadi Dj Choka

Mtanzania - - Swaggaz -

STAA wa singo ya Rafiki, Emmanuel Simwinga ‘Izzo Bizness’ amempa zawadi ya wimbo unaoitwa ‘Bila Sababu’, Dj mkongwe nchini, Hugoline Mtambachuo ‘Dj Choka’ kwa kupona maradhi ya Kifua Kikuu aliyoanza kuugua mwanzoni mwa mwaka huu. Akibonga na Showbiz, DJ Choka alisema ngoma hiyo inayotarajia kutoka mapema wiki ijayo ilikuwa ya Izzo B na alipoikuta studio za Uprise Music kwa prodyuza Dupy akaipenda, akaiomba na Bizness akampa kama zawadi.

“Huu wimbo niliukuta studio, ulirekodiwa kwa mara ya kwanza mwaka 2014, ulikuwa wa Izzo akimshirikisha Godzillah, wakati nasikilizishwa biti na mangoma ngoma nikakutana na huu wimbo, nikaupenda, nikauliza wa nani, Dupy akaniambia wa Izzo, nikawasiliana naye, akasema haina shida, ufanyiwe mixing upya, niingize sauti zangu, niuchukue kama zawadi ya birthday yangu na kupona maradhi ya Kifua Kikuu na kurudi kwenye muziki salama,” alisema Dj Choka.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.