KAMATASINGO 5 SINGO

ZINAZOHIT FLEVA BONGO FLEVA

Mtanzania - - Swaggaz - watazamaji laki saba ndani ya wiki mbili.

Hivi sasa Utaniua ya Jux ni wimbo ambao upo nafasi za juu kwenye chati mbalimbali za muziki ndani na nje ya Bongo. Utaniua ni ngoma kali, inayokua taratibu na inakimbiza kichizi kipindi hiki ambacho vuguvugu la King Kiba na MOND

VUGUVUGU la nyimbo mbili kutoka kambi hasimu za Rockstar 4000 kupitian goma ya Seduce me na Wasafi Classic Baby (WCB) na kibao Zilipendwa, lililoanza Agosti 25 mwaka huu limepungua. Bado Ali Kiba anaendelea kuongoza kwenye mtandao wa You Tube kupitia akaunti yake ya Vevo, tayari amefikisha watazamaji milioni 5.2 ndani ya siku 18 huku video ya Diamond Platnumz na wasanii wake ikitazamwa mara milioni 4.8 ndani ya muda huohuo. Uhasimu wa kambi hizo uliwagawa mashabiki na kufanya ngoma kali za wasanii wengine zisipate nafasi kubwa. Ushabiki huo ulifanya nyimbo za wasanii wengine zitulie,

zikae pembeni kidogo kupisha viguvugu hilo lililotawala kwenye mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari.

Hapa Swaggaz tunakusogezea ngoma tano kali ambazo ziliminywa na lile vuguvugu la Ali Kiba na Diamond na hivi sasa zina-hit taratibu na zinaendelea kufanya makubwa kwenye chati mbalimbali za muziki ndani na nje ya Bongo. ASLAY – PUSHA Hii ni ngoma ya tano kwa mwaka huu toka Aslay aanze kufanya kazi zake nje ya Yamoto Band. Alianza na Angekuona, Mhudumu, Baby, Likizo na Agosti 28 akaachia Pusha, wimbo ambao unafanya vizuri mtaani kuliko radio na runinga. Vuguguvu la Seduce Me na Zilipendwa lilifanya wimbo huu uonekane wa kawaida sana japokuwa hivi sasa ndiyo habari ya mjini. Unapanda chati kadiri muda unavyozidi kwenda, unakimbiza kwenye redio, televisheni na kitaa huku video yake ikiwa imefikisha JUX - UTANIUA Mkali Jux aliachia ngoma yake mpya, Utaniua siku moja kabla ya Ali Kiba na Diamond Platnumz hawajaachia mikwaju yao. Utaniua ni ngoma kali lakini ilishindwa kueleweka baada ya watu kutawaliwa na mizuka ya Seduce Me na Zilipendwa.

Hivi sasa Utaniua ya Jux ni wimbo ambao upo nafasi za juu kwenye chati mbalimbali za muziki ndani na nje ya Bongo. Utaniua ni ngoma kali, inayokua taratibu na inakimbiza kichizi kipindi hiki ambacho vuguvugu la King Kiba na Mond. CHEGE - RUNTOWN Ni ngoma inayofanya poa kwa sasa. Chege amekuwa na kawaida ya kuachia jiwe juu ya jiwe lakini alipoachia Runtown katika wiki ambayo kulikuwa na mvutano wa mashabiki wa Ali Kiba na Diamond, ilionekana ya kawaida. Lakini uzuri ni kwamba ngoma hii inaishi, inapenya taratibu na inaonekana kuendelea kufanya vizuri sana kipindi hiki ambacho vuguvugu la Seduce Me na Zilipendwa limepungua kwa kiasi kikubwa.

SAIDA KAROLO FT BELLE 9 & G Nako - Kichaka Baada ya kurudi kwa kishindo kwenye muziki, mwimbaji wa nyimbo za Asili Bongo, Saida Karoli aliachia wimbo wake unaoitwa Orugambo na Agosti Mosi, mwaka huu aliachia audio ya wimbo aliowashirikisha wanawe (Belle 9& G Nako) unaoitwa Kichaka. Aliusoma mchezo mapema, hivyo alisubiri mpaka vuguvugu la Zilipendwa na Seduce Me lipite ndiyo aachie video itakayofanya wimbo huo uwe hit kitaa, redio na runingani. Septemba 4, mwaka huu akaachia video ambayo imefanya wimbo huo uzidi kuwa mkubwa kadiri muda unavyozidi kwenda.

Ndani ya wiki moja tayari video hiyo imetazamwa na watu zaidi ya laki tatu. ROMA & STAMINA (Rostam) - Hivi Ama Vile Wimbo wa wakali hawa wa muziki wa rap Roma na Stamina unaoitwa Hivi Ama Vile, umeendelea kufanya vizuri zaidi kipindi hiki. Ulipotoka ulipokelewa vizuri lakini chati yake ilishuka baada ya ngoma za wababe wa Bongo Fleva kuachiliwa hewani. Lakini sasa wameibuka tena na singo yao inakimbiza kama kawa mtaani, redio na runingani.

Hizo ni baadhi tu ya nyimbo kali ambazo hivi sasa zinafanya vyema baada ya shughuli zote za muziki kusimamishwa na Kiba na Diamond wakichuana vikali kwenye vitu vyao Seduce Me na Zilipendwa.

Hii ni ngoma ya tano kwa mwaka huu toka Aslay aanze kufanya kazi zake nje ya Yamoto Band. Alianza na Angekuona, Mhudumu, Baby, Likizo na Agosti 28

Na SWAGGAZ

9&G Nako Kichaka Baada ya kurudi kwa kishindo kwenye muziki, mwimbaji wa nyimbo za Asili... SAIDA KAROLO FT BELLE

JUX - UTANIUA ASLAY – PUSHA ROMA & STAMINA

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.