Lima njegere, unavuna teke na kavu

Mtanzania - - Jiongeze - Husababishwa na fangasi Erysiphe polygoni. Mavuno ya punje kavu na kilo 1,500 kwa hekta.

Njegere ni miongoni wa mazao ya jamii ya mikunde inayolimwa katika maeneo ya ukanda wa juu.

Tanzania hulimwa zaidi Nyanda za Juu Kusini, Nyanda za Juu Kaskazini na kwenye miinuko ya Usambara na Uluguru.

AINA ZA NJEGERE

Pisum salivum Hizi hulimwa shambani, maua yake huwa meupe na mbegu zenye rangi ya kijani kibichi au njano nyepesi, hutumika kwa kuliwa punje kavu.

PISUM ARRENCES

Hulimwa bustanini, huwa na maua yenye rangi nyekundu/ zambarau. Mbegu huwa na rangi ya kijani kibichi au kijivu. Huvunwa kabla ya kukomaa kama mbogamboga, pia huhifadhiwa kwenye kopo.

Aina za njegere zinazopatikana nchini ni pamoja na Tanganyika yellow, Idaho white, Rondo na mbegu za kienyeji.

MATUMIZI YA NJEGERE

Punje teke hutumika kama mboga na ina protini nyingi, punje zilizokomaa na pia hutumika kwa chakula.

Mmea uliobaki hutumika kwa chakula cha mifugo, mbolea na kuhifadhi unyevunyevu ardhini. Hali ya Hewa Zao hili hustawi zaidi katika mazingira yenye hali ya ubaridi wa nyuzi 17 hadi 21.

Mwinuko zaidi ya mita 1,200 usawa wa bahari. Mvua na unyevu wa kutosha na maji yasiyotuama.

Udongo Njegere hukubali katika udongo uliowekwa mbolea, kulimwa kwa kina na wenye tindikali ya PH 5.5 – 6.5.

Utayarishaji wa shamba na kupanda

Shamba/bustani itayarishwe kwa kufuata mahitaji ya udongo kama kutotuamisha maji, kulimwa kwa kina.

Inashauriwa kupanda njegere mwanzo wa msimu wa mvua.

Nafasi za kupanda ni sentimita 60 hadi 90 kwa sentimita 5.7 kwa mbegu fupi.

Sentimita 12 hadi 15 kwa sentimita tano hadi 7.5 katika safu mbili za sentimita 90 kwa mbegu inayotambaa.

Njegere hustawi vizuri zikipata sehemu za kutambalia na huota baada ya siku saba hadi 10.

Njegere teke/mbichi hukomaa siku 60 – 90 na zile kavu huchukua siku 80 -150 kukomaa.

UTUNZAJI WA SHAMBA

Njegere hustawi vizuri katika shamba au bustani isiyo na magugu kwa kuwa magugu hushindana na kunyanganyana na mimea kutumia virutubisho. Pia huongeza kivuli wakati wa utoaji maua na kusababisha upungufu mkubwa wa mazao.

Palizi inatakiwa kufanyika kwa mkono au kutumia dawa za kuua magugu.

MBOLEA

Mazao yanayowekwa samadi hustawi vizuri. Katika kipindi cha ukuaji ni muhimu kuweka mbolea ya chumvichumvi za nitrogeni kwa kipimo cha kilo 40 kwa hekari.

WADUDU WAHARIBIFU

Wapo wadudu wengi ambao hushambulia zao la njegere baadhi yao ni American bollworm, Bean flies, Bean Aphids, Pea Aphids huambukiza virusi na Green peach aphids.

Magonjwa ni Ascochyta ambao hutokea kwa mabaka makubwa ya kahawia kwenye majani na matunda.

Pia hutokea hata kwenye shina. Katikati ya baka huwa rangi ya kijivu, kingo nyekundu/nyeupe husababishwa na fangasi aina ya Ascochyta pisi.

Ugonjwa mwingine ni Root Rot na Blight disease (kuoza kwa mizizi na Blingt), husababishwa na fangasi A. pinodella na mycosphaerella pinodes.

Dalili zake ni madoa madogomadogo yenye rangi ya zambarau/rangi ya kahawia iliyokaza au madoa meusi ambayo huungana na kusababisha jani na maua kuwa yenye rangi nyeusi.

Kuzuia tumia mbegu zisizo na magonjwa, zika mabaki ya mazao yaliyoadhirika kwa miaka mitatu hadi mine.

DOWNY MILDEW.

Dalili zake ni majani kuonekana kama yamemwagiwa unga na baadaye na kufa, Ugonjwa unaathiri zaidi mimea kipindi cha uhaba wa unyevunyevu. Kuzuia kwa kutumia sulphur ya unga kama inavyoshauriwa.

FUSARIUM WILT:

Husababishwa na fangasi/ ukungu Fusarium oxysporum, dalili zake ni majani kubadilika rangi kuwa manjano, mimea kudumaa, ugonjwa ukitokea kwenye mimea michanga huua mmea wote. Kuzuia tumia mbegu yenye uvumilivu kwa ugonjwa huu.

VIRUSI.

Mmea huonekana kuwa na uvimbeuvimbe kuzunguka jani, mmea hudumaa. Kuzuia kwa kutumia mbegu zisizo na maradhi.

UVUNAJI

Njegere teke huvunwa punje zikiwa bado mbichi. Uvunaji hufanyika mara mbili hadi tatu kwa wiki wakati wa kipindi cha ukuaji. Zaidi ya kilo 3,000 kwa heka za njegere teke huvunwa. Njegere kavu huvunwa wakati punje zimekauka na kuwa ngumu.

Ni muhimu kuwahi kuvuna njegere kavu ili kutopoteza mavuno zikipasuka.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.