FAHAMU NJIA ZA KUSTAWISHA MAGIMBI

Mtanzania - - Jiongeze -

SWALI: Habari ya kazi, nataka kujua magimbi yanaweza kustawi katika maeneo gani? Mimi naitwa Kungwe Sumaku nipo Mtwara Mikindani.

JIBU: Ndugu Sumaku, zao hili hustawi katik maeneo yenye kiasi cha nyuzi joto 25 hadi 30 na mwinuko wa mita 900 kutoka usawa wa bahari.

Magimbi hustawi katika eneo lenye ubaridi, unyevu na maeneo ya msitu. Aidha, hustawi katika eneo la tambarare au hata milimani, lakini zaidi katika maeneo ya bondeni au kwa kuotesha penye migomba, miti au kahawa ili kupata kivuli kwa sababu hayahitaji kupigwa na jua sana. UDONGO

Magimbi hustawi katika udongo tifutifu (loam soil). Udongo ni lazima uwe na rutuba ya asili ili kuleta mavuno mengi na yenye ubora. MBOLEA Zao la magimbi halihitaji mbolea nyingi. Kinachotakiwa ni kuotesha katika ardhi yenye rutuba ya asili kwa sababu ikiwekwa mbolea mara nyingi husababisha majani kumea na kushindwa kuweka viazi. Ikiwa ardhi haina rutuba yake ya asili basi waweza kuweka mbolea ya mboji kidogo hasa wakati wa kuandaa shamba. Sambaza mboji katika shamba zima ndipo ulilime, hii itasaidia udongo kuchanganyika vizuri na mbolea. MBEGU

Mbegu za magimbi hutokana na mzizi mkuu (tunguu) ambao huwa mnene na ndiyo unaobeba viazi au chipukizi ambao hujitokea pembezoni mwa shina.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.