Mexime abeba lawama kipigo Kagera Sugar

Mtanzania - - Michezo - Na MOHAMED KASSARA

KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Mexime, amesema yeye ndiye anastahili kubeba lawama baada ya timu hiyo kupoteza mchezo wake dhidi ya Azam FC.

Kagera ilikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Azam, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa juzi kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mexime alisema wachezaji wake walijituma na kucheza katika kiwango bora, huku wakitengeneza nafasi kadhaa za mabao, lakini bahati haikuwa upande wao, baada ya kujikuta wakifungwa bao hilo.

“Nawapongeza vijana wangu kwa mchezo mzuri waliouonyesha, licha ya kufungwa, tulijipanga vizuri na kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga, lakini bahati mbaya hutukufanikiwa kupata bao.

“Siwezi kuwalaumu wachezaji kwa hilo, lawama za kupoteza mchezo huo nitazibeba mimi mwenyewe, wachezaji walitimiza majukumu yao, kwa sasa mawazo tunayaelekeza katika kuhakikisha tunapata ushindi kwenye mchezo ujao,” alisema Mexime.

Kipigo hicho kinaifanya Kagera Sugar kubakia na pointi moja baada ya kucheza michezo mitatu, ilianza kwa kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Mbao FC, kabla ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Ruvu Shooting.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.