Dellilah:Naamini nitakuwa mke bora

Mtanzania - - Rose -

UHUSIANO ili usimame na kuwa na mafanikio unajengwa na vitu mbalimbali,vipo vinavyoonekana kwa macho ya watu na vingine ambavyo anaweza kuviona mtu uliyekuwa naye karibu pekee.

Dellilah Kessy ambaye amefunga ndoa na mchumba wake Jacob Mbuya anasema alikutana na mume wake miaka 2008 akiwa masomoni anasema talipoanza uhusiano na Jacob alikuwa anaamini ipo siku wata¿kia hatua ya kufunga..

Anasema katika maisha ya uhusiano kabla ya ndoa walikuwa wakizingatia zaidi mambo makuu matatu ambayo ni uvumilivu,uaminifu na heshima.

Anasema mbali na hilo pia wanawake wanapaswa kutambua kuwa mwanaume mwenye nia njema si lazima aanze kukutangazia vitu vizuri mwanzoni isipokuwa ataonyesha ishara ambazo kama mwanamke utahisi tu kuwa anakuhitaji katika maisha yake.

“Ukiwa na mtu katika uhusiano,maongezi mnayoongea na maisha mnayoishi unakuwa teyari umeshajua kama huyu upon a mtu mwenye nia gani,hivyo nilikuwa sina wasiwasi naye,”anasema Dellilah.

Anasema katika kipindi cha miaka tisa walichokuwa katika uhusiano wao waliishi kwa uaminifu,uvumilivu na kuheshimiana ili kuweza ku¿kia malengo waliyojiwekea

Anasema anaamini ndoa inapangwa na Mungu hivyo atamuongoza na kuwa mke bora kwa mume wake.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.