FILAMU

Mtanzania - - Rose - NA JOSEPH LINO

KIJANA Dylan Mitch Rapp (O’Brien) ni jasusi muuaji wa kimataifa aliyepoteza wazazi wake wote wawili katika ajali ya gari akiwa na umri wa miaka 14. Pia mpenzi wake anauawa katika mashambulizi ya kigaidi mara tu walipofunga uchumba.

Katika kutafuta njia ya kulipiza kisasi, anaajiriwa na Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA), Irene Kennedy (Lathan).

Irene anampa jasusi mkongwe, Stan Hurley kazi ya kumfundisha Mitch, ili baadaye kwa pamoja wachunguze wimbi la mashambulizi ya kigaidi yanayowalenga wanajeshi na raia.

Katika kufuatilia vurugu za mashambulizi hayo wanaungana na jasusi kutoka Uturuki, Annika (Negar), ili kukomesha mauaji katika kuanzisha vita ya dunia kwenye nchi za Mashariki ya Kati.

Hii ni filamu mpya ya American Assassin, imeongozwa na Michael Cuesta na kuandikwa na Stephen Schiff kutoka kwenye kitabu cha American Assassin, kulichoandikwa na Vince Flynn mwaka 2010.

America Assassin ilirekodiwa katika kipindi cha miezi matatu kuanzia Septemba hadi Desemba, mwaka jana, kwenye mji wa London, Birmingham (Uingereza), Rome (Italia), Phuket (Uturuki) na katika visiwa vya Malta.

Filamu hii imechezwa na Dylan O’Brien na Michael Keaton na imetengenezwa kwa bajeti ya dola milioni 40 na kuzinduliwa Septemba 15, mwaka huu nchini Marekani.

American Assassin tayari imeshaanza kuoneshwa katika kumbi za sinema nchini kote.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.