Jaji Mkuu David Maraga kung’olewa?

Mtanzania - - Jicho Pevu -

katika mkutano wa hadhara katika Soko la Burma, uliohudhuriwa na Rais Uhuru Kenyatta, Seneta Elgeyo Marakwet alitishia kushiriki mpango wa mabadiliko ya kikatiba ya kuifuta Mahakama ya Juu.

MVUTANO JUBILEE, NASA

Ni dhahiri kuwa, mivutano kati ya Chama cha Jubilee na muungano wa upinzani umefika kiwango cha juu kabla ya marudio ya uchaguzi Oktoba 17, mwaka huu.

Kiongozi wa Wabunge wa Chama cha Jubilee Bungeni, Aden Duale, ameongeza shinikizo la kumng’oa Jaji Mkuu, David Maraga iwapo muungano wa Nasa utaendelea na msimamo wake wa kutaka Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, Wafula Chebukati na Mkurugenzi wa Tume hiyo, Ezra Chiloba, wajiuzulu nafasi zao, basi nao watatumia wingi wao bungeni kumng’oa Jaji Maraga.

MAAGIZO YA KATIBA

Kwa mujibu wa wanasheria Emmanuel Nkoma na Ambroce Nkwera wa Finkleys Advocates ya jijini Dar es Salaam, walisema kuwa, “Nchi ya Kenya inapitia katika kipindi cha mpito cha kuonesha demokrasia ya kweli ndani na nje ya bara la Afrika. Ujasiri na msimamo wa Jaji Mkuu, David Maraga umeipa tasnia ya sheria uthubutu wa kulinda utawala wa sheria bila kujali nani ni nani. Hii imeonyesha pia kwamba kuwa mwanasiasa haina maana kwamba una nguvu kuliko wengine.

“Uamuzi wake haujawapendeza wapenda utawala usio wa sheria. Mbunge Ngunjiri Wambugu ambaye anajaribu kutaka Jaji MaraAkizungumza ga aondolewe kwenye kiti cha ujaji mkuu ni kujaribu kutaka kuitikisa tasnia ya utoaji haki.

“Kuna dhana ya uhuru wa mahakama (Independence of Judiciary) ambapo Majaji na mahakimu wanatakiwa kuwa huru wakati wa kutoa maamuzi bila kuingiliwa na upande wowote, yaani mihimili mingine ya dola, mfano Bunge na Serikali. Hatuoni kama ni jaribio ambalo linaweza kufanikiwa kwakuwa Kenya ina katiba nzuri ambayo inajali utawala wa sheria na si utawala wa kisiasa”.

Aidha, Finkleys Advocates wanaongeza kwa kusema: “Katiba inasema Jaji wa Mahakama ya Juu ataondolewa kwa sababu zifuatazo ambazo zipo kwenye Ibara ya 1 (a,b.,c,d,e) vinasema Jaji ataondolewa kwa; Kushindwa kutekeleza wajibu wake kutokana na matatizo ya kiakili au kiafya, ukiukwaji wa sheria (kuvunja sheria) zilizowekwa na Mahakama, kuwa na uwezo mdogo, ubadhirifu na ulaji rushwa na kufilisika.”

“Ibara ya 2 inasema kuondolewa yeyote kunatakiwa kufanywa na Tume ya huduma za Kimahakama au mtu yeyote kuwasilisha hoja katika Tume hiyo. Ibara ya 3(1 na 2) inasema hoja hiyo inatakiwa kuwa ya kimaandishi na kuonyesha vielelezo vya kutaka Jaji aondolewe. Ionyeshe makosa ya Jaji kwa mujibu wa vipengele vya kisheria.

“Ibara ya 4 inasema hoja binafsi za kumwondoa Jaji lazima zipitie kwenye Tume ya Mahakama na kutumwa kwa rais kwa mujibu wa Ibara ya 1. Ibara ya 5 inasema rais ndani ya siku 14 anatakiwa kumwondoa Jaji husika kwa mujibu wa mapendekezo ya Tume ya Huduma za Kimahakama.

“Ibara ya 5(a) hatua za kumng’oa Jaji Mkuu zinaweza; Spika wa Bunge kama mwenyekiti, Majaji watatu, wakili mmoja mwenye uzoefu wa miaka 14, na watu wengine wenye uzoefu na utumishi wa umma. Hizo ni sehemu chache, lakini Tume ya Huduma za Mahakama ndiyo wenye nguvu zaidi maana ndiyo inatoa hitimisho.”

Jaji Mkuu Maraga

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.