Kim Jongun apania viwango vya Marekani

Mtanzania - - Jicho Pevu -

KIONGOZI wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, ametangaza kuwa, lengo lake kuu kijeshi kwa sasa ni kuhakikisha linakuwa na uwezo sawa na lile la Marekani.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Korea Kaskazini, lilitoa taarifa hiyo baada ya kombora la majaribio la mwisho kufanywa, ikisema kuwa kiongozi wa taifa hilo, Kim Jong-Un, amesema hataki kusikia Marekani ikisema itakabiliana na Korea Kaskazini kijeshi.

Kiongozi wa taifa hilo, Kim Jong un, ameapa kuhakikisha kuwa taifa hilo linaafiki mpango wake wa kinyuklia kulingana na vyombo vya habari vya taifa hilo.

Lengo lake ni kuhakikisha jeshi la taifa hilo lina uwezo sawa na lile la Marekani, kulingana na chombo cha habari cha KCNA kilichomnukuu kiongozi huyo.

Matamshi ya Kim yanajiri baada ya taifa hilo kufanyia majaribio kombora lake kupitia anga ya Japan, likitajwa kuwa kombora lililosafiri kwa umbali mkubwa zaidi

Hatua hiyo imesababisha mgawanyiko miongoni mwa mataifa ambayo yaliungana nyuma ya Umoja wa Mataifa dhidi ya Korea Kaskazini siku chache zilizopita.

Lazima tuyaonyeshe mataifa yenye uwezo mkubwa vile taifa letu litakavyokamilisha mpango wake wa kinyuklia, licha ya vikwazo visivyoisha, Kim alinukuliwa na chambo cha habari cha KCNA.

Alisema kuwa, lengo la Korea Kaskazini ni kuwa na jeshi lenye uwezo sawa na lile la Marekani, ili kuwazuia watawala wa Marekani kutotaja suala la kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini.

Katika mkutano wa dharura, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliishutumu Korea Kaskazini kwa kufyatua kombora juu ya Japan, lakini likasisitiza kuwa hakutakuwepo na vikwazo zaidi dhidi ya taifa hilo.

Awali Marekani ilionya kuwa Korea Kaskazini itashambuliwa kijeshi iwapo vikwazo ilivyowekewa havitatekeleza chochote.

Lakini China kwa upande wake ilihimiza Marekani ikome kutoa vitisho na badala yake ianze kufanya mashauriano.

MAKAZI: Kambi ya Wakimbizi ya Lusenda iliyopo katika Mkoa wa Kivu Kusini nchini Jamahuri ya Kidemokrasia ya Kongo. PICHA NA DW.

Wanajeshi wa Korea kaskazini wakitoa heshima wakati wa kusherekee sikukuu ya ‘Day of the Sun’

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.