SIFA ZA VIWANJA 14 VINAVYOTIMKA VUMBI VPL 2017-18

Mtanzania - - Michezo - Na SOSTHENES NYONI -DAR ES SALAAM

LIGI Kuu Tanzania Bara, inayoshirikisha timu 16, inazidi kushika kasi.

Timu zinazoshindania taji hilo ni bingwa mtetezi Yanga SC, Simba SC, Azam FC, Mtibwa Sugar, Lipuli FC, Majimaji FC, Kagera Sugar, Mbao FC, Singida United, Ruvu Shooting, Mbeya City, Njombe Mji, Ndanda FC, Tanzania Prisons, Mwadui FC na Stand United.

Viwanja vitakavyotumika ni: Taifa,Jamhuri Dodoma, Sabasaba,Nangwanda, Majimaji, Azam Complex, Kambarage, Mwadui Complex, Sabasaba, CCM Kirumba, Sokoine, Manungu, Jamhuri Dodoma, Kaitaba na Mabatini.

MTANZANIA Jumapili linakuletea taarifa muhimu zinazohusiana na viwanja hivi;

1. Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

Uwanja huu ulianza kutumika mwaka 2007. Una vipimo vya mita 105 kwa mita 68 na milango 35 kwa ajili ya mashabiki kuingia na kutoka uwanjani. Una uwezo wa kuchukua zaidi ya mashabiki 57,000 waliokaa.

Klabu zitakazoutumia Uwanja huu kama uwanja wa nyumbani ni Simba na Yanga.

2. Uwanja wa Jamhuri, Dodoma

Uwanja huu upo katikati ya jiji la Dodoma, ukiwa unamilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Uwanja huu ulijengwa mwaka 1978, una uwezo wa kuchukua watazamaji 20,000.

Timu ya Singida United inautumia uwanja huu kama uwanja wake wa nyumbani.

Singida United, ambayo ina maskani yake Manispaa ya Singida, inautumia uwanja wa Jamhuri kama uwanja wake wa nyumbani, kwavile Uwanja wa Namfua, uliopo mjini Singida ambao ilipaswa kuwa, upo katika maboresho.

3. Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza

Uwanja wa Kirumba upo jijini Mwanza na unamilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Uwanja huu ulijengwa mwaka 1980 na una uwezo wa kuchukua watazamaji waliokaa 25,000. Uwanja huu utakuwa ukitumiwa na klabu ya Toto African ya Mwanza.

4. Uwanja wa Sokoine, Mbeya

Unapatikana katikati ya Jiji la Mbeya na ulijengwa mwaka 1977. Uwanja wa Sokoine una uwezo wa kuchukua mashabiki 21,000 na unamilikiwa na CCM.

Klabu ya Tanzania Prisons inayomilikiwa na Jeshi la Magereza na Mbeya City inayomilikiwa na Manispaa ya Mbeya zitautumia Uwanja huu kama uwanja wa nyumbani.

5. Uwanja wa Majimaji, Songea

Uwanja wa Majimaji upo katikati ya mji wa Songea, Mkoa wa Ruvuma na unamilikiwa na CCM. Ulijengwa mwaka 1979. Uwanja huu una uwezo wa kuchukua watazamaji 18,000 na utakuwa ukitumiwa na timu ya Majimaji kama uwanja wa nyumbani msimu huu.

Uwanja huu upo Manispaa ya Shinyanga na ulianza kutumika mwaka 1985. Una uwezo wa kuingiza watazamaji 15,000.

Uwanja huu ulipewa jina la Kambarage kama njia ya kumuenzi Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere.

Kama vilivyo viwanja vingi, pia unamilikiwa na CCM, klabu ya Stand United itautumia kama uwanja wake wa nyumbani.

7. Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara

Uwanja huu upo katika Manispaa ya Mtwara, eneo linalofahamika kama Umoja. Una uwezo wa kuchukua mashabiki 10,030 na una milango minne kwa ajili ya kuingia na kutoka uwanjani. Mmiliki wa Uwanja wa Nangwanda Sijaona ni CCM. Klabu ya Ndanda FC itautumia kama uwanja wake wa nyumbani.

8. Azam Complex, Dar es Salaam

Ujenzi wake ulianza mwaka 2010 chini ya mkandarasi Kampuni ya Salehe Msahala Contractors Limited. Azam Complex una uwezo wa kuingiza watazamaji 7,000.

Klabu zitakazoutumia Uwanja huu kama uwanja wa nyumbani ni Azam na JKT Ruvu. Mmiliki wa Uwanja huu ni Azam.

9. Uwanja wa Mwadui, Shinyanga

Ulijengwa mwaka 2010. Uwanja wa Mwadui una uwezo wa kuchukua mashabiki 5,000.

Mmiliki wa Uwanja huu unaopatikana ndani ya eneo la migodini ni wa Kampuni ya Diamond Petra. Klabu ya Mwadui FC itautumia kwa michezo ya nyumbani.

10.Uwanja wa Manungu, Morogoro

Uwanja huu ulijengwa mwaka 1988 na una uwezo wa kuchukua watazamaji 4,000. Mmiliki wake ni Kampuni ya Mtibwa Sugar. Klabu ya Mtibwa Sugar itautumia Uwanja huu kama uwanja wake wa nyumbani, lakini itakapokabiliana na Simba au Yanga itatumia Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, ambao ulijengwa mwaka 1978 na unamilikiwa na CCM. Jamhuri una uwezo wa kuchukua watazamaji 20,000.

11. Uwanja wa Samora, Iringa

Uwanja wa Samora upo mjini Iringa, ulijengwa mwaka 1975, unamilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Uwanja wa Samora unachukua watazamaji wapatao 25,000.

Timu ya Lipuli iliyopanda daraja msimu huu inautumia kama uwanja wake wa nyumbani.

12. Uwanja wa Kaitaba, Bukoba

Uwanja wa Kaitaba upo katika Mkoa wa Kagera, kando ya Ziwa Victoria, ni mali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Uwanja huu ulijengwa mwaka 1976, ukiwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 25,000.

Timu ya Kagera Sugar inautumia kama uwanja wake wa nyumbani.

13. Uwanja wa Sabasaba, Njombe

Uwanja huu unapatikana katika Mkoa wa Njombe. Una uwezo wa kuingiza mashabiki 7000.

Timu ya Njombe Mji ya mkoani humo ambayo imepanda daraja msimu huu inautumia kwa michezo yake ya nyumbani.

14. Uwanja wa Mabatini, Pwani

Uwanja huu unapatikana katika mji wa Mlandizi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani. Ulianza kutumika mwaka 2003.

Una uwezo wa kuchukua watazamaji 8000.

Timu ya Ruvu Shooting inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) inautumia kwaajili ya mechi zake za nyumbani.

Uwanja wa Samora, Iringa

Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam

Uwanja wa Jamuhuri, Dodoma

Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

Uwanja wa Kirumba, Mwanza

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.