Muwasho sehemu za siri

Mtanzania - - Rose -

M UWASHO ni aina ya ugonjwa unaowapata wanawake, ugonjwa huu unasababishwa na vitu vingi.

Sababu zinazochangia kuwashwa ni pamoja magonjwa wa zinaa, maambukizi ya fangasi ama matumizi ya maji yasiyo salama.

Sehemu nyeti (uke) huwa na bakteria wasa¿ ambao huishi katika uke kwa ajili ya sababu za kiafya. Hawa bakteria ndio wanaosaidia uke katika kupigana na wadudu wabaya wanapoingilia haya makao.

Lakini sasa, kama uke umetawaliwa na vijidudu wabaya, hii hali ya vijidudu wabaya husababisha kuwashwa kwa uke.

Na wakati mwingine kuwashwa huku huletea mtu kujisikia kama vile moto umewashwa, hasa wakati wa kwenda kukojoa (burning sensation) etc.

Pia magonjwa ya zinaa kama gonorea, kaswende n.k husababisha sehemu nyeti kuwasha.

Aina ya fungus aitwaye candida amekuwa maarufu sana kusababisha hali hiyo, huchangia kutoka kwa ute wa rangi nyeupe, njano au brauni ambayo huwa nzito. Na wakati mwingine hutoa harufu na pia kumfanya mtu ajisikie ananuka.

Fangasi inatibika na inapaswa kushughulikiwa mara tu mgonjwa apatapo ugonjwa huu, ni vizuri akamuone daktari ili ampe vidonge ambavyo ataingiza sehemu za siri au dawa ya kupaka.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.