Tuwapende, tuwalinde wanyama - Salome

Mtanzania - - Toto Kona -

T

ANZANIA ni kati ya nchi zilizobarikiwa kuwa na ardhi nzuri yenye rutuba na vivutio vingi, zikiwamo mbuga za wanyama.

Tembo ni miongoni mwa wanyama wenye thamani kubwa.

Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Ununio, iliyopo Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam, Salome Leonard (pichani), alizungumza na Totokona, wiki iliyopita, baada ya kushiriki kwenye matembezi ya hisani ya kupinga vita ya ujangili na biashara haramu ya pembe za ndovu.

“Wanafunzi tunapaswa kupewa elimu ya utunzaji wa mazingira na viumbe hai na visivyo hai, tunapaswa kuwapenda na kuwalinda wanyama,” anasema mwanafunzi huyo.

Salome anashauri kila shule kuwapo na utaratibu wa kuelimisha umuhimu wa kutunza na kuhifadhi wanyamapori.

“Wanafunzi tuelimishwe kuwa ni vibaya kuua aina yoyote ya mnyama kwa sababu mbali na shughuli za kitalii, pia tunaweza kuwatumia katika mafunzo kwa vitendo,” anasema Salome.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.