‘Kiingereza si somo la kuogopa’

Mtanzania - - Toto Kona - Na MANENO SELANYIKA

BAADHI ya wanafunzi wanaosoma shule za Serikali inadaiwa kuwa huwa wanakabiliwa na tatizo la kutoielewa vizuri lugha ya Kiingereza, tofauti na wale wa shule zinazomilikiwa na watu binafsi.

Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Uhuru Wasichana, iliyopo Ilala, Dar es Salaam, Ester Mabula, hivi karibuni alizungumza na Totokona na kusema mbali na changamoto ya uhaba wa walimu, pia wanafunzi wengi wanaiogopa lugha hiyo.

Ester anasema tatizo “wengi wetu hatuzingatii misamiati, kanuni za Kiingereza na kuzungumza mara kwa mara, Kiingereza si somo la kuliogopa kama utazingatia hayo”.

Mwanafunzi huyo anasema somohilo halimpi shida, kwa sababu huwa anamsikiliza kwa makini mwalimu wake na kusoma vitabu vya hadithi vyenye kuelimisha.

“Napenda kuongea na kuandika Kiingereza, ndiyo maana hata katika matokeo yangu ya mhula uliopita nilipata alama ‘A,” anasema mwanafunzi huyo.

Amewataka wanafunzi wenzake kufanya bidii katika masomo yote, likiwamo somo la Kiingereza.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.