Yus a Tuangalie katuni zenye kuelimisha

Mtanzania - - Toto Kona -

Na MANENO SELANYIKA

KATUNI ni kati ya vitu vinavyowavutia baadhi ya wanafunzi na hata watu wazima kuangalia. Licha ya kufurahisha na kuelimisha, hata hivyo, zipo katuni zenye taswira mbaya, hasa kwa watoto.

Wakizungumza na Totokona hivi karibuni, baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Uhuru Wasichana, iliyopo Manispaa ya Ilala, wamesema wanapenda kuangalia katuni, lakini zipo zinazofaa na zisizofaa kutazamwa na watoto.

Yusra Abas, mmoja kati ya wanafunzi hao, anasema: “Si kila katuni imetengenezwa kwa ajili ya kuangaliwa na wanafunzi, nyingine ni kwa ajili ya watu wazima.”

Mwanafunzi huyo anasema kupitia katuni baadhi ya wanafunzi hujifunza tabia za ugomvi na hata ukatili.

Yusra anawaasa wazazi kuzichunguza katuni kabla ya kuwapa watoto kuzitazama.

Yusra Abas (katikati), akiwa na wanafunzi wenzake wakiangalia michoro ya katuni kwenye kitabu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.