UTAWALA NDANI YA MIHIMILI MIWILI UTOFAUTISHWE

Mtanzania - - Mbele - Na HAFIDH KIDO

NAKUSUDIA kutoa elimu kidogo kuhusu mihimili ya dola, yaani Serikali, Mahakama na Bunge, ambayo kimsingi kila mmoja unajitegemea, hakuna mwingiliano. Kumekuwapo na mvutano kuhusu mhimili wa Mahakama kuingiliwa na Serikali kutokana na rais kuwa na mamlaka dhidi ya Jaji Mkuu ambaye kimsingi ni mtu mwenye mhimili wake.

Majirani zetu Kenya wameliepuka hili kutokana na Katiba yao mpya ambapo utaratibu wa kumpata Jaji Mkuu haumhusishi rais wa nchi. Ndiyo maana Jaji Mkuu wa Kenya, David Maraga, amemudu kusimamia kesi ya uchaguzi bila kigugumizi.

Turudi kwenye mada. Historia ya kuumbwa ulimwengu inatofautiana kulingana na imani au aina ya elimu uliyopata. Miaka ya nyuma zama za mawe wanadamu waliishi mbalimbali, hakukuwa na mataifa wala serikali.

Mataifa ya awali kujulikana ni Misri, India, China, Misapotamia (inahusisha Iraq, Syria, Jordan, Israel, Kuwait. Kwa kifupi ni Mashariki ya Kati katika miaka zaidi ya 600 kabla ya kuzaliwa Kristo), pia Taifa la Andes (Haya ni mataifa ya Marekani ya Kusini wakati huo ikiwa taifa moja).

Kazi kubwa ya wakazi wa mataifa haya ilikuwa ni waokota matunda na wawindaji, walikuwa wakiishi katika makundi madogo madogo kulingana na koo. Kila ukoo ukiwa na kiongozi wake na sheria zake.

Hata hivyo, baada ya ongezeko la watu na mahitaji koo zikaanza kupigana ili kupokonyana ardhi, wakati huo ardhi ikaanza kuwa ishara ya utajiri kwa sababu mahitaji kama maji, madini (chuma, dhahabu, almasi) yalihitajika kwa ajili ya uhunzi na mapambo.

Wakaanza kupambana, mwenye nguvu akamshinda dhaifu, kisha akawa chini ya utawala wake. Wataalamu wa historia wanaeleza katika miaka hiyo watawala wakaanza kuheshimika kama miungu.

Kutokana na kiburi cha madaraka, kama tulivyoona kwa Farao wa Misri.

Watawala wengi walijinasibu kuwa wamepewa utawala na Mungu, wanaongoza kwa utashi wa kidini na hata Ukristo ulipotawala duniani haikuonekana tofauti baina ya Kanisa na Serikali.

Kwa sababu masuala mengi ya Kikanisa yaliingizwa kwenye utaratibu wa kiserikali. Mfano mzuri ni Julius Caesar alikuwa mkuu wa dini katika Roman State Religion. Hata hivyo, katika miaka ya 1642 na 1651 kulitokea vita ya wenyewe kwa wenyewe Uingereza. Ilipewa jina la vita ya wote dhidi ya wote: ‘War of all against all.’

Mwanafalsafa Thomas Hobbes akaandika kitabu ikiwa ni ushauri kwa watawala kuweka silaha chini na kukubaliana namna ya kuongoza, kuwa na mikataba ya kijamii kuhusu utawala. Andiko hili aliliita Leviathan.

Hobbes alisema vita ya wenyewe kwa wenyewe inaweza tu kuondolewa kwa kuweka serikali madhubuti. Wananchi waweke silaha chini na kukubali kutawaliwa, lakini wapewe ahadi ya amani na utulivu. Ndiyo maana majeshi ya polisi duniani kote kazi yao ni kulinda mali na raia.

Hata hivyo, mbali ya kuwepo na serikali zilizo na mamlaka, lakini bado makanisa ndiyo yalikuwa na nguvu ya kuamua nani awe kiongozi na nani asiwe kiongozi. Baadhi liliwakera hili.

Mwanafalsafa St. Augustine aliandika kitabu cha kusifia utawala wa kanisa katika mataifa, alikiita “The City of God”. Ameeleza mengi, ikiwamo mfano wake kuwa kiongozi wa dunia anachaguliwa mbinguni.

Anasema ikiwa wanadamu watakuwa na utulivu duniani kwa kuwasikiliza viongozi wao, maana yake wataupata ufalme wa Mungu. Kwa miaka kadhaa wafalme waliongoza kwa kutumia miongozo ya Kanisa (Divine right). Wafalme walionekana ni watawala wa serikali na Kanisa, mfumo huu uliitwa (Caesaropapism). Papa alikuwa na

Majirani zetu Kenya wameliepuka hili kutokana na Katiba yao mpya ambapo utaratibu wa kumpata Jaji Mkuu haumhusishi rais wa nchi. Ndiyo maana Jaji Mkuu wa Kenya, David Maraga, amemudu kusimamia kesi ya uchaguzi bila kigugumizi.

sautikubwa katika serikali nyingi duniani. Katika miaka ya 1500, Martin Luther, aliyezaliwa mwaka 1483 na kufariki 1546, aliwafungua watu akilikutokana na utaratibu huu. Alikuwa muasi katika Kanisa Kana ndiye anayetajwa kuwa mwasisi wa Kanisa la Kiluteri. Lutheran Church, Tanzania linaitwa Kanisa La Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT. Andiko lake la ‘The Two KingDoctrine’ doms Doctrine liliamsha wengi kuhusiana na haja ya kujitenga Kanisa na Dola. Alisema kuna tambili ndani ya utawala mmozima ja, lazima itofautishwe. Katika miakaya 1530, Mfalme Henry VIII wa England alitofautiana na Papa Clement VII, ikawa kuna ugomvi bainaya Kanisa na Dola, hivyo Mfalme akawa ndiye kiongozi wa kanisa, Church of England. Tangu miaka hiyo ya Mfalme Henry VIII, wafalme wa England wanakuwa na cheo cha ‘Supreme Governor of the Church of England.’ Vilevile kama wanafalsafa wengine wa miaka hiyo, John Locke, raia wa England (16321704), alipigia kelele suala la kuanywa changanywa dola na kanisa. Andiko lake pia ndilo lililoathiri katibaya Marekani na hoja zilizo wazi kuwa kuchanganya Kanisa na Dola kunaathiriunaathiri kwa kiasi kikubwa umaniza watu na viongozi. Moja ya watu waliopiga kelele katika miaka hiyo ni Denis Diderot, mwanafala safa wa Ufaransa aliyezaliwa mwaka 1713, aliandika: ‘The distance between the throne and the altar can never be too great.’ (Umbali kati ya kiti (ufalme) na madhabahu (sehemu ya kuabudia) haitakiwi kuwatukufu (kubwa). Kalele zilikuwa kubwa za kutaka Kanisa na Dola visiingiliane, Rais wa tatu wa Marekani, Thomas Jef, ferson, alipata kuandika barua kwa Taasisi ya Danbury Baptist, hii ilikuwa taasisi iliyojumuisha makanisa zaidi ya 26 Marekani. linala barua hiyo maarufu ilini kuwa ni ukuta wa kutenganisha kanisa na dola. Hiyo ilikuwa mwa2. ka 1802. Tafsiri yangu: “Naungana nanyi kuwa dini ni suala linaloegeati mea kati ya mtu na Mungu wake, kwamba mtu yeyote anawiwa na iminayake au ibada yake, kuwa mguyuya serikali inafikia maamuzi pekeena si maoni. Nafikiri mamlaDola ka ya kwa watu wa Marekani yanayobainisha kuwa Bunge lao halitakiwa kuunda sheria itakaysu oruhusu kuundwa dini au kuzuia wananchi kuabudu watakavyo, ndiyo maana tunajenga ukuta kuanisa zuia Kanisa na Dola”. Mbali ya juhudi hizo, hadi sasa katika katiba ya Marekani hakuna kipengele kinachobainisha kutoha fautisha Kanisa na Dola, ingawa marais wengi wamekuwa wakioa nyesha kutounga mkono kuingiliwana Kanisa. Rais aliyepata umaarufu nchini humo, John F. Kennedy, mwaka 1960 alipata kusema: “Naamini katika Amerika ambapo kutoha fautisha shughuli za Kanisa na Dola ni suala la msingi, ambapo hakuna kiongozi wa Kanisa Katoliki atakayeweza kumwambia rais (Mkatoliki) namna ya kuongoza, wala Mchungaji wa Kiprotestanti anayeweza kumwambia mfuasi wake nani wa kumpigia kura kwenye uchaguzi wa kisiasa, ambapo hakuna kanisa au shule ya kanisa inayopokea ruzuku ya serikali au msaada wa kisiasa.

“Wala hakuna mtu atakayenyimwa kazi katika ofisi ya serikali kwa sababu tu imani yake inatofautiana na imani ya rais ambaye anaweza kumteua au kuchaguliwa kwa kura.

“Naamini ndani ya Amerika kuwa si Mkatoliki, Mprotestanti wala Myahudi ambaye ni ofisa wa serikali anayeombwa au kupokea maagizo kuhusiana na sera za serikali kutoka kwa Papa, Baraza la Taifa la Kanisa au chanzo chochote cha kanisa, ambapo hakuna chombo chochote cha dini kinachotaka kuingiza sheria zake dhahiri au kwa siri dhidi ya jamii yote, wala hakuna dini inayopewa mamlaka makubwa kiasi kutendewa kinyume kwa kanisa moja ni kutendewa kinyume kwa jamii nzima.” (Tafsiri ni yangu).

Mataifa mengine kama Brazil, Italia, Ufaransa na Uingereza kama tulivyoitaja hapo juu, bado yanaendelea na utaratibu wa kutambua au kupambana kujitenga na Kanisa. Kwa mfano, Katiba ya Brazil tangu mwaka 1988 inazuia mwingiliano wa masuala ya kikanisa katika Dola, katiba inatamka wazi kuzuia kuanzishwa kwa kanisa ndani ya Dola, wala viongozi kujikurubisha na masuala ya kidini.

Tanganyika ilipopata uhuru mwaka 1961, ilitamka wazi si taifa la kidini, maana yake si kanisa wala msikiti wala sinagogi itakayoingilia mamlaka ya Dola, lakini wananchi wake wana dini. Ufaransa katika katiba yake iliyoundwa mwaka 1905 ina kipengele wanakiita laïcité, kinatamka wazi kujitenga kanisa na Dola wala viongozi wake kujikurubisha na masuala ya kiimani.

Italia katika ibara ya 7 ya Katiba yao kinatamka wazi: “Dola na Kanisa Katoliki vinajitegemea na vina mamlaka yake na maamuzi. Uhusiano wake unasimamiwa na Lateran pacts (Mkataba wa Lateran 1929 kati ya Italia na Holly See unaweza kugoogle). Mabadiliko ya mkataba huo ambayo yanakubaliwa na pande zote mbili hayatakiwi kuhusisha mabadiliko ya kikatiba.”

(Tafsiri ni yangu).

Hata hivyo, Uingereza, mbali ya historia ya kujitenga kati ya kanisa na Dola, bado kanisa Anglikana ina mamlaka makubwa, ikiwamo kusimamia shughuli za kusimikwa watawala na pia wawakilishi wa kanisa wana viti maalumu katika mafunzo ya kidini na Maaskofu 26 wana viti katika Baraza la Mabwanyenye (House of Lords) ambapo wanatambulika kama Lords Spiritual.

Makala haya yametokana na utafiti wa kimtandao na vitabu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.