HIGH LOW BADO INATAMBA

GAUNI za high low bado hazijashuka kwenye mzunguko wa fasheni duniani.

Mtanzania - - Mbele -

GAUNI za high low bado hazijashuka kwenye mzunguko wa fasheni duniani. Bado ni vazi linaloweza kushonwa tofauti na likakufanya uwe gumzo kwa kuvutia wale wanaoliona.

Ndivyo ilivyo kwa Rihanna, ambaye mwezi Julai mwaka huu na mwezi huu alivaa vazi hilo katika mishono na rangi tofauti alipohudhuria haÀa mbili tofauti.

Katika haÀa ya onesho la ¿lamu la Valerian Premiere lililofanyika Los Angeles, Marekani mwezi Julai, alivaa gauni la mtindo wa tulle (kama ambavyo niliwahi kuuandika hapa) lenye rangi ya pinki likiwa na mkato wa high low (mbele fupi, nyuma refu) na off shoulder (bila bega).

Mshono huo wa Rihanna uliwavutia wengi, huku wengine hapa nchini wakiuiga. Mmoja wa walioshonewa nguo kama ya Rihanna ni Miss Tanzania wa mwaka 1998, Basila Mwanukuzi.

Basila alishonewa gauni hilo la rangi ya bluu na House of Stylish, iliyochini ya msanii Jaqueline Wolper.

Wolper pia alimshonea mke wa Said Fella, maarufu Mkubwa Fella, gauni ambalo lilikosolewa zaidi kutokana na kutovutia kwa mvaaji huyo.

Wiki hii, Rihanna alivaa tena gauni la rangi nyeusi ambalo ni high low lililobuniwa na jumba la mbunifu mkubwa duniani, Ralph & Russo Couture.

Gauni hilo alilivaa Alhamisi hii wakati wa haÀa ya mfuko wake wa hisani wa Clara Lionel Foundation, unaotumika kusaidia jamii mbalimbali.

Rihanna pia alivaa choker shingoni iliyofunika vyema na kuendana na mkato wa nguo yake.

Bracelet ni moja ya urembo ambao msanii huyo hupenda kuvaa.

Kiatu alichovaa Rihanna katika gauni lake la high low jeusi. Ni kiatu chenye malighafi ya ngozi.

Cheni ambazo Rihanna alivaa na gauni jeusi. Zipo za madini tofauti ikiwemo almasi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.