Fahamu cha kufanya kwa mpenzi mwenye hasira -2

Mtanzania - - Habari -

WIKI iliyopita tulianza kuangalia makala haya ya kufahamu nini ufanye kwa mpenzi mwenye hasira. Endelea ilikoishia .... J izuie usiombe msamaha au kumtaka radhi Najua watu wengi, hususani jinsia ya kike waki¿kia hatua hii hujiona wao ndio wakosaji na hivyo kukimbilia kuomba radhi. Kumbuka kuwa mpenzi mkoro¿ na mtukanaji hastahili kuombwa radhi. Nikweli yawezekana wewe ni sababu kwa kiasi fulani kwa tatizo hilo lakini kwa kule kukasirika kwa staili hiyo hakumfanyi astahili kuombwa radhi maana kwa kufanya hivyo utaendeleza tabia yake hiyo mbaya. Msamaha au radhi yaweza ikafaa baadae kidogo wakati mpenzi wako ametulia na ameiweza hasira yake. Jaribu kuiihifadhi samahani yako mpaka wakati huo u¿ke. Mpongeze mpenzi wako mara tu anapoamua kufanya lile lenye staha na wala siyo anapoonyesha hasira. Wakati wowote mpenzi wako anapoonyesha kushuka na kuelewa kuwa analofanya sio jema, mpongeze, mtiemoyo aendelee na tabia hiyo njema kwa kumwonyesha utayari wa kumsikiliza kile anachotaka kusema ili m¿kie maa¿kiano. Katika mahusiano jifunzeni kuzipongeza na kuzitia moyo tabia na matendo mema na pia kuyazuia yale yasiyomema yasiendelee. Jipongeze pia Kamwe usiruhusu matukano, kejeli na kasfa za mpenzi wako zikuvunje moyo na kukushusha thamani yako. Usijione mnyonge kwa lawama zake labda tu uchague kukubali anachokisema kwako. Jione bado kuwa wewe ni mwema na ulikuwa unafanya mambo kwa nia njema. Ukiweza jipongeze kwa kufanya kile ambacho hisia zako zitaona zimepongezwa. Mfano, jitoe mtoko, nenda kwenye ¿lamu, jipikie kitu kizuri, fanya nafsi yako ijisikie iko juu. Kama unajiona kuwa huwezi au unapata shida zaidi kuzifuata njia hizi basi jitahidi kumtafuta mshauri wa kisaikolojia “counselor” kwa msaada zaidi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.