Fedha haikufanyi kuwa baba bora

Mtanzania - - Habari -

MALEZI ya wazazi wawili yanatajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kupata watoto wenye maadili.

Kauli hii haimaanishi kwamba watoto wanaolelewa na mzazi mmoja hawana maadili, hapana, isipokuwa wataalamu wa saikolojia ya malezi wanataja malezi ya baba na mama yana afya zaidi.

Katika malezi kila mzazi ana nafasi yake, pamoja na mama kuwa kiungo muhimu, hata hivyo baba naye ana nafasi kubwa katika kumjenga mtoto.

Baadhi ya watu wanadhani baba anahitajika zaidi katika nafasi ya kifedha tu.

Mtazamo huo si sawa, kwa kuwa baba ni nguzo na ufunguo wa mtoto kupata ujasiri wa maisha, si kwamba mama hawezi kuyafanya hayo, bali kwa kiwango chake hawezi kum¿kia baba.

Ladha ya baba inapatikana kwa baba mwenyewe, baba anahusika katika malezi na makuzi ya mtoto.

Baba ni kichwa cha familia, lakini pia ni mhusika mkuu anayetakiwa kutengeneza mfumo mzuri wa familia.

Kipimo cha kuwa baba bora si uwezo wa kifedha, si umbile na wala sauti yake, bali ni uwezo wa kutengeneza mfumo mzuri wa mahusiano kati yake, mke na mtoto wake.

Kwa nafasi aliyonayo baba anaweza kujenga nguzo za ndoa kama amani, upendo, maendeleo na uwajibikaji ambao utazaa familia bora siku za usoni.

Maelewano yaliyopo ndani ya nyumba baina ya wazazi kwa kuongozwa na mwanamume yanaweza kumjengea mtoto picha nzuri ama mbaya katika ukuaji.

Ili mtoto aweze kuwa na msingi mzuri, ni muhimu baba kutenga utaratibu wa kuwa na muda mzuri wa kukaa na watoto, akili ya mtoto mdogo hutafsiri na kutambua mapenzi ya mtu fulani kwakuangalia zaidi muda anaompa.

Suala la kutenga muda kwa watoto huwa linawashinda zaidi wanaume, kutokana na aina ya maisha wanayoishi ambayo yanazingatia zaidi ratiba za kutafuta fedha.

Wataalamu wa masuala ya malezi wanashauri hata kama ukiwa na mambo mengi kiasi gani, baba anatakiwa kujua kuwa na muda na familia, hasa watoto.

Kukaa karibu na watoto kunasaidia kupata nafasi ya kujua jinsi wanavyoishi na matatizo yao.

Pia watoto hujifunza mambo mengi kupitia baba zao, wapo ambao wanakuwa katika nafasi nzuri katika maisha, kwani hata uwepo wake na baba pia anaweza kuyajua mengi ya watoto wake na hata kuyarekebisha au kuyaboresha.

Baba tenga muda mzuri wa kuongea na mwanao ili uweze kumjenga kuwa kijana mwema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.