Boresha siku yako kwa vazi bora

Mtanzania - - Jicho Pevu -

MAVAZI ni kitu cha kuangalia kwa umakini wa hali ya juu. Kupitia vazi lako unaweza kuharibu siku yako kutokana na uchaguzi wako wa vazi la siku hiyo.

Ni kweli kuna siku hujisikii kuvaa vazi la aina fulani lakini unapaswa kuwa makini na uchaguzi wako kwa kuhakikisha kuwa ulilochagua ni bora na si ilimladi vazi.

Hii huwakumba zaidi watu ambao kila siku wanakwenda makazini yaani wafanyakazi ambao kuna wakati hujikuta wakichoka kuchagua.

Lakini pia wapo ambao huvaa sare za o¿si wanayofanyia kazi hivyo kujikuta wakati mwingine unachukia vazi hilo.

Haina maana kuwa ukiwa mfanyakazi ambaye sare ya o¿sini kwako ni suti basi uvae suti ilimladi hata kama ni ya zamani, unaweza kuiboresha utakavyo.

Mavazi yanaweza kukuvuta kufanya kazi zaidi. Ukizingatia haya yatakusaidia kuboresha;

Upekee

Haijalishi kazi yako, jione kuwa ulivyo ni kitu kikubwa na unaweza kufanya hivyo kupitia chochote ukivaacho. Jaribu kuboresha mavazi yako ya kazini kwa kuongeza vikolombwezo kama cheni, saa na pochi nzuri.

Ingizo jipya

Wapo wanaopenda kuvaa kila ingizo jipya la nguo, kama wewe ni mmoja wao basi endelea lakini jaribu kuwa na nguo za kipekee zaidi.

Ubunifu

Hilo ni jambo muhimu ambalo unapaswa kulifanya. Mfano wa hilo unaweza kuwa na top au blauzi za aina moja za kazini lakini ukaongeza skafu, mkanda, au koti.

Rangi

Usiogope rangi, unaweza kuvaa rangi unayoona huiwezi lakini ukapendeza zaidi.

Vutia

Usivae kitu ili mradi umejistiri, jaribu kuvaa nguo itakayokuvutia kwanza mwenyewe na kukufanya kuwa na ujasiri machoni mwa wengine.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.