Butiku: Nyerere hakuwa mjinga kufa masikini

Mtanzania - - Mbele - Na EVANS MAGEGE

MWENYEKITI wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amesema, Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, hakuwa mjinga kufa masikini.

Butiku alitoa kauli hiyo Dar es Salaam jana wakati akichangia maada kwenye kongamano la Kibweta cha Mwalimu Nyerere kilichoandaliwa na Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni.

Maada kuu ya kongamano hilo ilisema, “Mtazamo wa Mwalimu Nyerere katika Uchumi wa Viwanda na Maendeleo ya Jamii”.

Akichangia, Butiku alisema Nyerere alikuwa muumini wa usawa hivyo alijituma kuweka misingi ya maendeleo kwa utaifa wa Watanzania wote.

Alisema kama Baba wa Taifa angekuwa na moyo wa ubinafsi na mroho wa mali, angeanza kwa kujilimbikizia mali kabla ya maendeleo ya nchi na asingekufa masikini.

Alisema Nyerere aliona mbali katika kuleta maendeleo yenye usawa kwa wananchi kwa kuanzisha viwanda.

Butiku alisema kwa sasa yapo malengo ya kuanzisha viwanda kama alivyofanya Baba wa Taifa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.