Rick Ross ampa tena shavu Diamond

Mtanzania - - Habari - Na CHRISTOPHER MSEKENA

BAADA ya kupata ubalozi wa mvinyo wa Luc Belaire, staa wa singo ya Hallelujah, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, ameendelea kutusua kwenye anga la kimataifa baada ya kutua Marekani kukamilisha kolabo yake na balozi mwenzake wa kilevi hicho, rapa Rick Ross.

Meneja wa msanii huyo, Babu Tale, alitumia ukurasa wake wa Instagram kuwataarifu mashabiki wa Diamond Platnumz kuwa, kuna ngoma mpya aliyomshirikisha bosi wa lebo ya Maybach Music Group, Rick Ross inakuja, ambayo juzi ilikuwa inafanyiwa video jijini Miami, Florida.

“Kuthubutu ni sehemu ya kufanya, dhamira yetu ni kuupeleka muziki wa Bongo Fleva mbali, kikubwa ni dua zenu,” aliandika Babu Tale jana, baada ya kuweka picha akiwa na Diamond na Rick Ross wakifanya video ya kolabo hiyo ambayo inaongozwa na mwongozaji mkongwe kutoka nchini Uingereza, Mr Moe Musa, aliyefanya video ya Hallelujah.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.