Katibu Chadema Shinyanga afariki dunia kanisani

Mtanzania - - Kanda - Na SAM BAHARI

ALIYEKUWA Katibu wa Chama cha Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Shinyanga, George Kitalama aliyefariki dunia kwa shinikizo la damu amezikwa

Mwenyekiti wa Chadema Wilaya hiyo, Tutis Jilungu alisema katibu huyo alifariki dunia Jumapili akiwa katika Kanisa Kuu la Kiinjili la Kulutheri (KKKT) mjini Shinyanga akishiriki kikao cha kamati ya utendaji ya kanisa hilo.

Alisema kabla ya kwenda katika kikao hicho, Kitalama alikuwa akihuhudumia watoto kwa kuwapatia bidhaa mbalimbali pamoja chakula kilichoandaliwa kwa ajili yao na kanisa.

Kitalama enzi ya uhai wake aliwahi kuwa diwani wa Kata ya Kitangili katika Manispaa ya Shinyanga tangu mwaka 2010 hadi 2015.

Alisema pamoja na wadhifa huo pia aliwahi kuwa Katibu wa Chadema Wilaya ya Shinyanga tangu mwaka 2015 hadi januari mwaka 2017.

Jilungu alisema Kitalama alizaliwa mwaka 1966 katika Kijiji cha Isanzu, Wilaya ya Mkalama Mkoa wa Singida.

Mwili wa marehemu uliagwa katika Kanisa la KKKT na kusafirishwa kwenda kijijini kwao Mkalama kwa mazishi ambayo yaliyofanyika juzi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.