Waajiri 10,000 wasubiriwa kujiandikisha WCF

Mtanzania - - Kanda - Na MASYENENE DAMIAN

WAAJIRI 10,000 kutoka taasisi na mashirika ya serikali hawajajiandikisha katika Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), imefahamika.

Hatua hiyo itawawezesha wafanyakazi wao kunufaika na huduma za matibabu na fidia nyngine zijazotokana na malipo ya ajali kazini.

Waajiri 10702 wamekwisha kujisajili kwenye mfuko huo tangu mwaka jana, huku sekta binafsi ikiwa ina mwitikio mdogo.

Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Masha Mshomba amewahimiza kujisajiri kuwapa haki waajiriwa wao kwa sababu wamekuwa wakipata usumbufu watumishi wao wanapopata na majanga kazini.

Alikuwa akifungua mafunzo ya siku tano kwa madaktari na waganga wa hospitali na vituo vya afya kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa jijini Mwanza.

Mafunzo hayo maalum ni kwa ajili ya kutathmini ajali na magonjwa yatokanayo na kazi kwa wanufaika wake na yalihusisha madaktari 409.

Mshomba alisema mfuko huo umelipa fidia ya Sh milioni 867 kwa mwaka wa fedha 2016/17 kwa wafanyakazi waliopata ajali kazini.

“Lengo letu ni kulipa fidia sahihi na kwa wakati, kwa hiyo mfuko huu umekuja kwa wakati muafaka hivyo ni muhimu waajiri kujisajili na kuwapa haki waajiriwa waweze kunufaika.

“Kwa mwaka wa fedha ulioisha tumelipa fidia ya Sh milioni 867 kwa wafanyakazi kama gharama za matibabu ya ajali na magonjwa yanayotokana na kazi na malipo ya ulemavu kwa kila mwezi.

“Hii ni kwa wale waliopata matatizo kuanzia Julai mosi mwaka jana,” alisema.

Mshomba alisema mfuko huo una wanachama zaidi ya milioni moja kutoka sekta binafsi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.