Romanus Mwangi'ngo: Uzagaaji wa majitaka utakuwa historia

Mtanzania - - Jamii Na Afya - Na TUNU NASSOR -DAR ES SALAAM

SERIKALI kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji inaendelea kuboresha hali ya usafi wa mazingira kwa kuongeza uwezo wa mfumo wa ukusanyaji na usafishaji wa majitaka katika jiji la Dar es Salaam.

Maandalizi ya awamu ya kwanza ya mpango huo yameanza baada ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) kukabidhiwa eneo la Jangwani ambapo mtambo wa kwanza wa kisasa wa kusafisha majitaka utajengwa.

Mradi huu ni sehemu ya mkakati wa Serikali kuongeza uwezo wa mfumo wa ukusanyaji na usafishaji wa majitaka katika jiji la

Dar es Salaam ambapo lengo ni kulaza kilometa 563 za mabomba ya ukubwa mbalimbali ya ukusanyaji majitaka yatakayokusanya majitaka na kuyamwaga katika mitambo mikubwa mitatu itakayojengwa Jangwani, Kurasini na Mbezi.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwangi’ngo, anasema mitambo hiyo mipya itatumika kuzalisha gesi asilia na umeme kwa ajili ya kujiendesha, hivyo kupunguza matumizi na gharama za umeme kwenye mradi huo.

Anasema maji yatakayokuwa yamesafishwa yatauzwa na kutumika katika shughuli mbalimbali kama vile kupozea mitambo na umwagiliaji na tope litakalobaki baada ya mchakato huo wa usafishaji litatumika kama mbolea kwa ajili ya kilimo.

Katika eneo la Jangwani, bustani ya kisasa itakayokuwa na miti ya kivuli, maua na viti vya kupumzikia itatengenezwa ili kuboresha taswira ya eneo hilo.

Mwangi’ngo anasema mradi huo unahusu ujenzi wa mtambo wa kusafisha majitaka eneo la Jangwani na utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kusafisha mita za ujazo 200,000 kwa siku.

Mfumo wa mabomba yenye urefu wa kilometa 376 yatakayolazwa kuanzia

Ubungo hadi Jangwani, Kinondoni, Mwananyamala, Msasani, katikati ya jiji na Ilala utajengwa.

Awamu ya kwanza ya ujenzi itahusisha mtambo utakaoweza kusafisha mita za ujazo 25,000 za majitaka kwa siku na mabomba ya kilometa 17.43 yatakayojengwa katika mitaa ya eneo la Magomeni.

Katika awamu hii ya kwanza bomba linalomwaga majitaka baharini

litaacha kutumika na badala yake majitaka hayo yatakwenda kusafishiwa katika mtambo huo.

Kuhusu mfumo wa majitaka Mbezi Beach, Mwang’ingo anasema Majitaka yakiwa yamezagaa katika moja ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam

mradi huo unahusu ujenzi wa mtambo wa kusafisha majitaka utakaojengwa eneo la

Kilongawima ambapo ukikamilika utakuwa na uwezo wa kusafisha mita za ujazo 16,000 kwa siku na utajumuisha mfumo wenye urefu wa kilometa 97 utakaojengwa katika eneo la Mbezi Beach, Kawe,

Kilongawima, Tegeta na maeneo mengine jirani. Mradi huo utajengwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia kupitia mkopo wa masharti nafuu na unatarajiwa

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.