Masoko ya moja kwa moja kuchochea ujasiriamali - QNET

Mtanzania - - Jamii Na Afya - Na Mwandishi wetu -DAR ES SALAAM

TABAKA la kati la Tanzania linakuwa kwa kasi hali ambayo inalazimisha uwiano sawa wa ukuaji wa mahitaji ya bidhaa zilizotengenezwa maalumu katika daraja la juu na huduma ambazo zitakidhi mahitaji yao mbalimbali.

Huduma mpya ijulikanayo kama ‘kid on the clack’ ambayo inaweza kuja kuziba pengo la mauzo ya moja kwa moja, mwenendo ambao umekuwa ukifanyika kwa miaka mingi sasa na ambao umepewa nguvu ya msukumo na kamapuni ya masoko ya kiulimwengu kutoka Asia (QNET), ambayo hivi karibuni imefungua biashara zake nchini.

Mfumo huu wa mauzo unazipatia kampuni njia mbadala ya kusambaza na kuuza bidhaa zao na huduma zao moja kwa moja kwa wateja, tofauti na mfumo au utaratibu uliozoeleka wa kuuza rejareja sehemu moja.

Sekta hii inatumia aina mablimbali za mbinu za usambazaji na miongoni mwao ni masoko ya matabaka mbalimbali na masoko ya mtandao.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa ofisi ya QNET nchini, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dk. Adelhlem Meru, alizidhibitishia kampuni kuhusu hali nzuri ya utulivu ya mazingira ya kibiashara na masoko yaliyopo kwa ajili ya bidhaa na huduma zake.

“Mazingira mazuri yanawezeshwa na sera nzuri ambazo zimewekwa na serikali zinazohamasisha uwekezaji wa moja kwa moja wa wazawa na wageni.

“Uchumi unaokuwa kwa kasi ambao unatoa uhakika wa fursa endelevu za kukua kwa biashara na hali ya amani inayoendelea nchini ambayo ni kiungo muhimu kwa ajili ya maendeleo ya ujasiriamali na maendeleo yoyote,” anasema Dk. Meru.

Kwa mujibu wa QNET, bidhaa za biashara za mtandao zinazotolewa zinajumuisha aina tofauti za mitindo ya maisha ya kiulimwengu na bidhaa za kiafya kama vile huduma binafsi, virutubisho, vipodozi, huduma za nyumbani, nguvu za maji, vito na saa za mkononi pamoja na vifurishi vya sikukuu.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangala, anasema sera ya serikali ni kuhakikisha kwamba Watanzania wanafurahia kiwango cha juu cha huduma, hivyo wana imani na bidhaa za QNET ambazo zimekidhi viwango.

“Tuko tayari kusaidia kampuni ambazo zina nia njema kwa Watanzania,” anasema Dk. Kigwangalla.

Mfumo wa Mauzo ya moja kwa moja unajivunia wazo la biashara la kimataifa na linaelezwa kama mauzo ya bidhaa na huduma moja kwa moja kwa watumiaji, mtu kwa mtu, mbali na maduka ya kuuza rejareja yaliko.

Mfumo huu wa mauzo una umri wa zaidi ya miaka 100 na mwanzo kabisa mfumo huu ulianzia USA. Leo, hii ni sekta yenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 180 duniani na ambayo ina karibu watu milioni 90 wanaohusika katika biashara hii.

“QNET inaona fahari kuwa Tanzania na imejidhatiti kufanya kazi kwa karibu zaidi na serikali na kujenga fursa zaidi za ujasiriamali kwa ajili jamii. Mauzo ya moja kwa moja yanawapatia watu fursa kubwa ya kujiunga katika ujasiriamali,” anasema Sharma, Mshauri katika bodi ya wakurugenzi ya QNET.

Mfumo wa mauzo ya moja kwa moja unatoa uwezo kwa mtu binafsi kujitengenezea kipato kwa kupitia kujiajiri yeye mwenyewe na kufanya kazi kwa bidii.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.