Ndoa, mimba za utotoni bado ‘mfupa mgumu’

Mtanzania - - Jamii Na Afya - Inatoka vii

45, Tabora asilimia 43, Dodoma asilimia 39, Mara asilimia 37 na Shinyanga asilimia 34,” anabainisha.

Tafiti zaidi Mkurugenzi huyo anasema utafiti wa Afya ya Uzazi na Utoto na Viashiria vya Malaria (TDHS) wa mwaka 2015 unaonyesha, asilimia 27% ya watoto wa kike wanapata mimba wakiwa na umri chini ya miaka 18.

“Aidha, taarifa ya utafiti ya hali ya ukatili dhidi ya watoto iliyotolewa mwaka 2011 unaonyesha, kwa kila watoto wa kike watatu, mtoto mmoja sawa na asilimia 27.9 amefanyiwa vitendo vya ukatili,” anasema.

Mussai anaongeza “Kwa mujibu wa utafiti huo, asilimia 6.9 walilazimishwa kufanyiwa ukatili wa kingono, wizara kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo tulitumia siku hiyo kufanya shughuli mbalimbali ikiwamo kutoa elimu ya kujitambua na afya ya uzazi ili watoto wa kike waweze kujilinda na mimba za utotoni.

Anasema walifanya uhamasishaji kujenga uelewa kwa waendesha bodaboda kuhusu madhara ya ndoa za utotoni na kujali utu wa mtoto wa kike.

“Kauli mbiu ya mwaka huu ilikuwa ‘Tokomeza Mimba za Utotoni; Tufikie Uchumi wa Viwanda’ ambayo kimsingi ililenga kuweka msisitizo kwa jamii kupiga vita kwa nguvu zote mila na desturi zenye athari kwa watoto zenye kupelekea mimba za utotoni na kuathiri maendeleo hasa ya mtoto wa kike na hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya nchi kwa ujumla,” anasema.

Anaongeza “Kuna usemi kwamba kumwendeleza mtoto wa kike ni kuendeleza familia na Taifa, kwa sababu mchango wa mwanamke katika uchumi wa nchi ni mkubwa kwa

kuzingatia idadi ya wanawake ukilinganisha na wanaume hapa nchini.

“Kundi hili lina mchango mkubwa katika ujenzi na maendeleo ya viwanda nchini. Hivyo tabia na mienendo yote yenye viashiria vya kusababisha mimba kwa watoto wa kike ni lazima vidhibitiwe. Hii itasaidia kuwa na watoto watakaowezesha Taifa kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ifikapo mwaka 2030,” anasisitiza. Utekelezaji

Mussai anasema katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili watoto wa kike Serikali kwa kushirikiana na wadau imeanza kutekeleza Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (2017/18 -2021/22). “Mpango huu umelenga kupunguza ukatili dhidi ya watoto kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2021/22 na tunatarajia kupunguza mimba za utotoni kutoka asilimia 27 hadi kufikia asilimia tano,” anasema.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto wa wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Margaret Mussai .

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.