Eco-Village kupanda miti 5,000

Mtanzania - - Kanda - Na ODACE RWIMO

MRADI wa Eco-village unaotekelezwa wilayani Igunga kuboresha mazingira katika kupanda miti na majiko sanifu umewezesha kupanda miti 5,000 wilayani humo.

Mradi huo unaotekelezwa na Shirika la Heifer International Tanzania huwashirikisha wadau mbalimbali wakiwamo wanafunzi kujifunza namna ya utunzaji bora wa mazingira.,

Walimu na wanafunzi kutoka shule 13 walipongeza hatua hiyo juzi walipofanya ziara maalumu a kutembelea miradi ya utunzaji mazingira inayofadhiriwa shirika hilo.

Walisema elimu, hamasa na utaalamu unaotolewa na maofisa wa mradi huo umewezesha kupandwa miti zaidi ya 5000 katika maeneo mbalimbali ya kata za Mbutu na Igunga wilayani humo.

Mmoja wa walimu hao, Faustin Francis kutoka Shule ya Msingi Bukama, alisema elimu ya kupanda miti waliyopewa na wataalamu wa Igunga Eco-village imeiwezesha shule yao kupanda miti zaidi ya 900.

Alisema hivi sasa mandhari ya shule yameanza kupendeza baada ya kupata utaalamu wa kuotesha, kupanda na kutunza miti hiyo.

Mwalimu Oswald Simba kutoka Shule ya Msingi ya Mtakatifu Leo Mkuu, alisema maeneo mengi ya wilaya hiyo ni jangwa.

Alisema lakini mandhari ya sasa ya Kijiji cha Bukama, Mwang’halanga na baadhi ya shule yanavutia kwa sababu ya kuanzishwa upandaji miti unaoratibiwa na Eco-Village.

“Tunatoa pongezi nyingi sana kwa mradi wa Igunga Eco-village umerejesha uoto wa asili uliopotea katika wilaya nzima ya Igunga.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.