Ashindwa kutetea nafasi yake

Mtanzania - - Kanda -

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Vijijini, Mwenzetu Mgeja, ameshindwa kutetea nafasi yake baada ya kuangushwa na Edward Ngelela kwa kura 109 katika uchaguzi wa chama hicho, anaripoti Sam Buhari.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Msimamizi wa Uchaguzi huo, Paul Makolo alimtangaza Edward Ngelela kuwa mshindi wa nafasi ya uenyekiti baada ya kupata kura 433 na kumshinda mpinzani wake wa karibu Mwenzetu Ngelela aliyepata kura 324.

Alisema kwa nafasi ya Katibu Mwenezi, Emmanuel Lukanda aliibuka mshindi baada ya kupata kura 107 na kumshinda mpinzani wake Nuhu Manoni aliyepata kura 13 na Kasimu Adamu akiambulia kura mbili.

“Kwa matokeo haya Edward Ngelela atakuwa mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga vijijini kwa miaka mitano ijayo na Katibu Mwenezi atakuwa Emmanuel Lukanda ,” alisema Makolo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.