DC awapongeza wahasibu

Mtanzania - - Kanda -

MKUU wa Wilaya ya Kaliua, Abel Busalama, amewapongeza watumishi wa idara ya uhasibu katika halmashauri ya wilaya hiyo kwa umakini mkubwa katika kuandaa taarifa za hesabu za mapato na matumizi ya halmashauri, anaripoti Odace Rwimo.

Busalama alitoa pongezi hizo akiwa amefuatana na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Haruna Kasele na Mbunge wa Kaliua, John Kadutu (CCM) katika kikao maalumu cha baraza la madiwani.

Alisema ripoti ya mwaka wa fedha 2016/17 iliyoandaliwa na wataalamu wa fedha na kuwasilishwa na Mweka Hazina, Costa Mzanye, imefafanua vema na kuweka wazi mapato, matumizi na madeni yote ya halmashauri hiyo.

Alisema taarifa za fedha za umma zinatakiwa ziandaliwe kwa uwazi na weledi mkubwa huku zikifafanua na kuondoa utata na kujibu maswali yote ya ukaguzi iwe kwa wakaguzi wa ndani au wa nje.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.