Wafafanua zawadi ya magari

Mtanzania - - Kanda -

MKURUGENZI Mtendaji wa Shule za Msingi na Sekondari za Waja zilizopo Mkoa wa Geita, Wambura Chacha, amefafanua sababu za kuwazawadia wanafunzi wa sekondari waliofanya vizuri katika mitihani yao zawadi ya magari, ANARIPOTI HARRIETH MANDARI.

Chacha alisema ameamua kuwazawadia gari kwa kuwa itawasaidia kuwarahisishia usafiri kuwahi masomo yao ya elimu ya juu.

Alisema pia itawahamasisha wanafunzi wengine kuongeza bidii kwenye masomo yao hivyo kupata ufaulu mzuri katika matokeo ya mtihani wa mwisho.

Chacha aliwazawadia wanafunzi wawili, Biera Kabaruka na Edna Meela, magari yenye thamani ya Sh milioni 10 kila moja wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.