Waziri achangia mabati

Mtanzania - - Kanda -

NAIBU Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (pichani) amechangia mabati 170 yenye thamani ya Sh milioni 2.7 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Mwandete wilayani Maswa, ANARIPOTI SAMWEL MWANGA

Nyongo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki (CCM) alisema amekabidhi msaada huo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa kwa wananchi wa kijiji hicho baada ya kumjulisha kuwa wameanzisha ujenzi huo.

Alisema mkakati wake kwa sasa katika sekta ya afya ni kuboresha huduma za afya kwa kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na zahanati katika jimbo hilo kuwawezesha wananchi kupata matibabu karibu na makazi yao.

Alisema ni lazima wananchi washiriki katika kutatua changamoto zinazowakabili katika maeneo yao na siyo kusubiri kila jambo kuwa litafanywa na serikali au viongozi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.