Serikali yaagiza hati ya shamba irejeshwe

Mtanzania - - Kanda - Na SAFINA SARWATT

SERIKALI ya Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, imeagiza kurejeshwa kwa hati miliki ya shamba la ushirika wa Uru Kati, ili liweze kupangiwa matumizi mengine.

Agizo hilo lilitolewa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba, wakati akizungumza na viongozi wa ushirika huo.

“Kuna maeneo ambayo yana migogoro na shughuli za maendeleo zimekwama kutokana na kuwapo kwa migogoro ya ardhi.

“Kwa hiyo, naagiza hati hii irudishwe mara moja ofisini kwangu ili maeneo ambayo hayana mgogoro yaweze kupimwa ili shughuli za kimaendeleo ziendelee.

“Kwa mujibu wa maelezo na vielelezo mbalimbali, ardhi ile ilikuwa ni ya ushirika na wanaushirika waligawa sehemu ya ardhi hiyo na kuipa Shule ya Uru Seminari, ekari 40,” alisema Kippi.

Kwa upande wake, mmoja wa wanaodai eneo hilo, Dominic Mbararia, ambaye pia ni Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Ushirika Uru Mawela, alisema madai yao ni ya msingi na yanalenga kuleta maendeleo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.