Wakulima wa chai kujengewa barabara

Mtanzania - - Habari -

WAKULIMA wa chai mkoani Njombe wamehakikishiwa ifikapo Machi mwakani, watakuwa na barabara bora zinazopita mashambani na kuwarahisishia kufikisha mazao yao kiwandani kabla hayajaharibika.

Ikiwa ni sehemu ya ziara iliyofanywa hivi karibuni na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Kilimo, Mifugo na Maji mkoani Njombe, Mhandisi Ali Mwinchande ambaye ni Meneja Miradi ya Miundombinu Ofisi ya Jumuiya ya Nchi za Umoja wa Ulaya Tanzania, alisema tayari fedha zimeshatengwa kwa ajili ya kukarabati baadhi ya barabara ndani ya mikoa mitatu ambayo ni Iringa, Njombe na Mbeya.

“EU ni mdau mkubwa wa maendeleo ya Tanzania na tunaunga mkono sekta ya kilimo. Mwaka huu kuna mradi unaandaliwa kwa ajili ya kuboresha na kuendeleza kilimo katika mazao ya chai, kahawa na mboga mboga,” alisema Mwinchande.

Alisema kwa mwaka huu wa fedha wametenga Sh bilioni 127.2 kwa ajili ya barabara na kwamba ndani ya miaka mitano ijayo EU imejipanga kutumia Euro milioni 140 katika sekta ya kilimo na barabara.

“Eneo hili la Njombe ni la mvua nyingi kwa hiyo kila mwaka itakuwa tunakarabati upya barabara. Tutaangalia barabara gani zinatakiwa kuwa katika kiwango cha saruji au lami lakini si changarawe tena.

“Hadi mwezi wa tatu mwakani tutakuwa tumeshaanza kuita wakandarasi kwa ajili ya kujenga. Mwaka ujao wa fedha tayari utakuwa tumeshapata ufumbuzi wa matatizo haya yanayowakabili wakulima,” alisema. Awali, Meneja wa Kampuni ya kuhudumia wakulima wadogo wa chai mkoani Njombe (NOSC), Filbert Kavia, alizungumzia kwa uchungu ubovu wa barabara mbele ya wajumbe wa Kamati na Waziri wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba, katika shamba linalomilikiwa na kampuni hiyo.

“Kwa kawaida majani ya chai yanatakiwa kufika kiwandani muda mfupi tu baada ya kuchumwa, yakichelewa yanaharibika na kwa bahati mbaya majani ya chai yakishaharibika huwezi hata kulishia mifugo hayana kazi tena.

“Ubovu wa barabara unarudisha nyuma maendeleo ya wakulima wadogo ambao kwa kiasi kikubwa kipato chao kinatokana na kazi hii,” alisema.

TUZO: Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao ( katikati) akikabidhiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Aggrey & Clifford, Rashid Tenga, tuzo ya kimataifa ya dhahabu kutoka Spike Asia Festival of Creativity 2017 nchini Singapore iliyotokana na tangazo lililotengenezwa na kampuni hiyo kwa niaba ya Vodacom kuhusu kampeni ya kuuza sehemu ya hisa za kampuni hiyo kwa umma, Dar es Salaam jana.Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia. – PICHA: MPIGAPICHA WETU

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.