Ecobank yaboresha huduma zake

Mtanzania - - Habari -

BENKI ya Ecobank imeendelea kuboresha huduma zake za kiteknolojia kwa wateja wake nchi mbalimbali za Afrika.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana katika mkutano uliowakutanisha wafanyakazi na wafanyabiashara, Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo, Mwanahiba Mzee, alisema huduma zilizoboreshwa ni pamoja na huduma ya ‘mobile banking’.

Alisema huduma nyingine iliyoboreshwa ni ya kumjali mteja kwa wakati mwafaka pale anapohitaji huduma kwa haraka.

Alisema wamekutana na wafanyabiashara na wateja wa benki hiyo, ili kujua changamoto wanazokumbana nazo katika biashara zao wakati wakiwa ndani na nje ya nchi.

“Licha ya kuwepo kwa huduma hizi tangu awali, lakini tumeona ni vyema tukapata mrejesho kutoka kwa wateja wetu ili kujua changamoto wanazokumbana nazo ili tuweze kuzifanyia kazi,” alisema.

Mmoja wa mteja wa benki hiyo, Godfrey Mogela, alisema amejifunza mengi kutokana na huduma zinazotolewa na benki hiyo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.