Mbao FC, Mbeya City hapatoshi

Mtanzania - - Michezo -

TIMU ya Mbao FC inatarajiwa kushuka dimbani leo kuvaana na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, unaotarajiwa kufanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Katika mchezo wa mwisho, Mbao ilitoka sare ya kufungana bao 1-1 na Prisons, wakati Mbeya City ilitoka sare ya kufungana mabao 2-2 na Mwadui. Mbao FC inashika nafasi ya tisa kwenye msimamo ikiwa na pointi 5, huku wapinzani wao Mbeya City wakishikilia nafasi ya 7 kwa kujikusanyia pointi saba.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kocha mkuu wa Mbao FC, Ettiene Ndayiragije, alisema kikosi chake kilikuwa na matatizo katika safu ya ushambuliaji, lakini tayari amefanikiwa kufanya maboresho.

Ndayiragije alisema amefanikiwa kumaliza tatizo la wachezaji kukosa kasi na kupoteza nafasi za wazi za kujipatia mabao, ambalo lilionekana kwenye mchezo wao uliopita.

“Ninaamini mazoezi ambayo tumeyafanya kwa kipindi hiki cha wiki moja, ambapo timu zilikuwa kwenye mapumziko mafupi yatakuwa yamekisaidia kikosi chake,” alisema Ndayiragije.

Ndayiragije alisema matarajio yake ni kuishuhudia timu yake ikiutumia vema uwanja wa nyumbani kuvuna pointi na mabao, ambayo yatawapa nafasi ya kupanda juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu.

Mchezaji wa timu ya mpira wa wavu ya Jeshi Stars, Zuhura Hassan (kushoto), akipiaga mpira kuelekea upande wa timu ya APR ya Rwanda wakati wa michuano ya kumuenzi Mwalimu Nyerere Dar es Salaam jana. – PICHA:JUMANNE JUMA

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.