Yanga yaibadilishia gia Kagera Sugar

Mtanzania - - Michezo - Na MOHAMED KASSARA

KAMA Kagera Sugar walitega mashushushu wake kwa ajili ya kuifanyia fitina Yanga itakapotua Mwanza kabla ya kuelekea Bukoba kwa usafiri wa basi, watakuwa wamefeli kwani mabingwa hao watetezi wamebadili gia angani na kuamua kupanda ndege hadi mkoani Kagera.

Awali, kikosi hicho cha Yanga kilikuwa kisafiri kwa ndege hadi Mwanza kisha kuchukua basi hadi Bukoba, lakini baada ya kupima upepo na kubaini huenda wakafanyiwa fitina wameamua kubadilisha mawazo hayo na kuamua kupanda ndege ya moja kwa moja.

Yanga inachukua tahadhari ili kuepuka mizengwe kutoka kwa Kagera Sugar wanaoburuza mkia wakiwa na pointi mbili katika msimamo wa ligi hiyo baada ya kucheza mechi tano.

Kikosi cha Yanga kinachonolewa na kocha Mzambia George Lwandamina, kipo katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi hiyo kikiwa nafasi ya sita kwa kujikusanyia pointi tisa ikiwa imecheza mechi tano nyuma ya watani wao timu ya Simba walio kileleni mwa ligi hiyo wakiwa na pointi 11.

Msafara wa wachezaji 27 wa Yanga na viongozi wa benchi la ufundi unatarajia kuwasili Bukoba leo, siku moja kabla ya kuvaana na Kagera Sugar katika Uwanja wa Kaitaba.

Mchezaji wa timu ya Morogoro Sisters, Gloria Mussa (kulia), akimiliki mpira huku akizongwa na mchezaji wa Kisarawe Queens, Veronica John, wakati wa mechi ya Ligi ya Wanawake iliyofanyika katika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam jana. Morogoro imeshinda...

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.