Bilioni 1.6/- zayeyuka Z’bar

Mtanzania - - Habari - Na MWANDISHI WETU -ZANZIBAR

TUME iliyoundwa na serikali kuchunguza ufisadi wa fedha za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imebaini upotevu wa zaidi ya Shilingi Bilioni 1.6.

Taarifa ya kubainika kwa upotevu huo ilitolewa jana na Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar, Dk. Khalid Mohammed Salum katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyikia ofisini kwake. Waziri Salum alisema taarifa ya tume hiyo inatofautiana na ya awali iliyotolewa na wizara yake ikieleza kuwa hadi Juni mwaka 2016, kulikuwa na upotevu wa Sh milioni 571.030 za serikali.

“Tume imefanya kazi yake, imechunguza na kubaini kuwa kiasi cha fedha zilizopotea zinafikia au kuzidi shilingi bilioni 1.619. “Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango iliunda tume ya uchunguzi wa kadhia hii kama sheria inavyoelekeza na tume baada ya kumaliza kazi yake ilijiridhisha kwamba kuna upotevu wa fedha unaokisiwa kufikia au kuzidi shilingi bilioni 1.619,” alisema Dk. Salum.

Alisema katika uchunguzi huo, tume ilibaini kuwa afisa mmoja kati ya 12 waliosimamishwa kupitisha uchunguzi hawakuhusika na upotevu huo na imependekeza warejeshwe kazini.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.