Umasikini unachangia utapiamlo

Mtanzania - - Habari - Na ASHURA KAZINJA - MOROGORO

UMASIKINI umetajwa kuwa chanzo kikubwa kwa watu kutokula mlo wenye lishe ya kutosheleza ambao una virutubishi vya kutosha vyenye vitamini na madini vinavyohitajika katika mwili wa binadamu.

Hali hiyo imepelekea utapiamlo au njaa iliyofichikana ambayo husababishwa na ukosefu wa muda mrefu wa vitamini na madini muhimu yanayohitajika kwa ajili ya ukuaji kikamilifu na maendeleo ya mwili ambao unawaathiri zaidi watoto na wajawazito, huku ikiwa ni vigumu kumjua kwa dalili mtu mwenye njaa iliyofichikana.

Kutokana na hilo, Mradi wa Kapu la Mazao Lishe (BNFB) unaohimiza uwekezaji na ulaji vyakula vyenye wingi wa vitamini na madini wakishirikiana na Kituo cha Kimataifa cha Viazi (CIP) chenye makao makuu nchini Peru, wameanzisha mradi utakaosaidia kutokomeza njaa iliyofichikana kwa kuzalisha mazao yenye viini lishe unaodhaminiwa na Bill & Melinda Gate.

Akizungumza na MTANZANIA, Mratibu Mwandamizi wa Mradi wa Kapu la Mazao Lishe, Dk. Richard Kasuga, alisema mradi huo umejikita katika kupambana na njaa iliyofichika kwa kutumia mkusanyiko wa vyakula mbalimbali vyenye viini lishe kama viazi lishe, mahindi ya njano, mihogo na maharage ili kumrahisishia mwananchi wa kawaida mwenye hali ya chini kuzalisha mwenyewe.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.