Uongozi halmashauri ya Buhigwe wapongezwa

Mtanzania - - Kanda - Na EDITHA KARLO

KATIBU Tawala wa Wilaya ya Buhigwe, Peter Masindi amewaomba viongozi wapya wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe kuhakikisha wanaenda na kasi ya awamu ya tano.

Aliwashauri waiongoze halmshauri hiyo kwa kasi ya maendeleo na kuibua miradi mbalimbali itakayoongeza pato.

Masindi alikuwa akizugumza katika Kikao cha baraza la madiwani la kufunga mwaka 2016-2017 la halmashauri hiyo.

Alisema vingozi waliochaguliwa wanapaswa kuwa kichocheo cha maendeleo na kuwaeleza kuwa wanao wajibu wa kuanzisha mchakato wa ujenzi wa madarasa ya shule, ujenzi wa hospitali ya wilaya na kuibua miradi mbalimbali itakayosaidia kuongeza kasi ya makusanyo ya mpato kwa halmashauri.

“Niwaombe tuongeze kasi ya maendeleo na ili tufanikiwe ni lazima tushikamane tuungane kuwa kitu kimoja bila ya kujali itikadi za vyama vyetu.

“Tuna changamoto kubwa ya kuhakikisha tunapata maendeleo na wanachi wakafurahia uongozi huu ambao leo mmeupata kwa kuchaguliwa na madiwani wenzenu,” alisema.

Katika uchaguzi huo nafasi ya Mwenyekiti wa Halmashauri ilichukuliwa na Venace Kigwinya (CCM) huku Makamu Mwenyekiti akishinda Hamisi Lukanka (CCM).

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe, Anosta Nyamoga aliwapongeza viongozi hao waliochaguliwa na kuwaomba kufanya kazi kwa kushirikiana na wataalamu.

Alisema hategemei kuibuka migogoro wala maneno bali utandaji kazi.

Alisema Baraza la Madiwani lina wajumbe 27 na wote walijitokeza kupiga kura uchaguzi ulikuwa huru na wa haki.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Buhigwe, Venace Kigwinya aliwashukuru madiwani hao na kuendeleza ushirikiano na kuachana na makundi na mgawanyiko wa vyama.

Aliwashauri wafanye kazi kwa ushirikiano kuhakikisha halmashauri hiyo inasonga mbele na kupata mafanikio zaidi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.