TAMU, CHUNGU BIASHARA MADUKA MAKUBWA NCHINI

Biashara Tanzania kuongezeka mara mbili kufikia 2050

Mtanzania - - Biashara Na Uchumi - Na JOSEPH LINO

MADUKA makubwa ya rejareja (Supermarkets) ni washirika wakubwa wenye uwezo katika maendeleo ya viwanda na maisha ya kila siku.

Biashara ya maduka nchini imeendelea kukua katika miaka ya hivi karibuni na imekuwa ikitengeneza bei za ushindani na upatikanaji wa bidhaa na huduma mbalimbali kutokana na ukuaji wa miji na mabadiliko katika tabia ya ununuzi.

Ikiwa ni sehemu ya kuwa na maisha bora kwa Watanzania ambao wengi wanajibidiisha katika shughuli mbalimbali za kilimo na ujasiriamali ambao huwapatia kipato wanachotumia kwenye gharama mbalimbali za maisha. Mazingira haya yamekuwa yakivutia wawekezaji kutoka nje kufanya biashara nchini hasa katika Jiji la Dar es Salaam ambapo maduka makubwa (supermarkets) yapo mengi.

Watu wenye maduka hayo wamekuwa wakiwekeza nchini baadaye kufanya biashara, lakini baada ya muda si mrefu na kutokana na sababu mbalimbali zisizofahamika yanashindwa kujiendesha na mbaya zaidi hukumbwa na malimbikizo ya madeni na hivyo kusababisha kusuasua huduma katika soko.

Inaendelea Uk. vi

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.