Madiwani wazuia fedha kugawiwa usiku

Mtanzania - - Kanda - Na IBRAHIM YASSIN

MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba mkoani Songwe, wamepiga marufuku kitendo cha maofisa wa mpango wa kusaidia kaya masikini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf), kugawa fedha kwa wanufaika nyakati za usiku kwa madai kuwa kitendo hicho ni hatari.

Akizungumza mwishoni mwa wiki wakati wa kikao cha wazi cha baraza la madiwani kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo, Diwani wa Kata ya Chitete, Levis Siyame, alisema amepokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wanufaika hasa wazee kuhusu kuwepo kwa ugawaji wa fedha usiku wa manane.

Diwani wa Kata ya Nzowa, Cledo Mwaipopo, alisema suala la ugawaji wa fedha usiku wa manane limekuwa likifanyika kata nyingi ikiwamo Nzowa.

Alisema ugawaji wa fedha hizo, kunaashiria kuweka mazingira mabaya ya wanufaika kuvamiwa, kujeruhiwa na hata kuuawa kisha kuporwa fedha kutoka kwa watu wenye nia ya kujipatia fedha kwa njia za kuwadhuru watu kwa kuwavamia hivyo aliomba suala hilo lifanyike mchana ili kulinda usalama wa watu.

Naye Kaimu Mratibu wa Tasaf wilayani humo, Rose Sanga, licha ya kukiri kuwapo ugawaji huo, alisema imetokana na jiografia ya sehemu hiyo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Mathew Chikoti, alimwagiza mkurugenzi kulifanyia kazi suala hilo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.